• HABARI MPYA

    Tuesday, November 29, 2016

    NASSOR 'FATHER' MWENYEKITI MPYA AZAM FC

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    ALIYEKUWA Makamu Mwenyekiti wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Nassor Idrissa 'Father', ameteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa timu hiyo akirithi mikoba ya Alhaji Said Mohamed Abeid, aliyefariki dunia mwanzoni mwa mwezi huu.
    Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, na kuituma kwenda kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwafahamisha mabadiliko hayo, imeeleza kuwa Shani Christoms Mligo, ndiye atakuwa Makamu Mwenyekiti mpya wa timu hiyo akichukua nafasi ya Idrissa.
    Mabadiliko hayo ya kiuongozi yamefanywa na Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC, ambapo uteuzi huo umeanza rasmi leo Novemba 29 mwaka huu.

    Nassor Idrissa 'Father' (kulia), ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Azam kufuatia kifo cha Alhaji Said Mohamed Abeid, aliyefariki dunia mwanzoni mwa mwezi huu
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NASSOR 'FATHER' MWENYEKITI MPYA AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top