• HABARI MPYA

    Tuesday, November 22, 2016

    MBEYA CITY YAJIVUNIA MAKIPA WAKE WADOGO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MBEYA City imesema kwamba ina hazina ya makipa watatu vijana, ambao kama wataendelea na juhudi ya mazoezi watafika mbali.
    Ofisa Habari wa Mbeya City, Dismass Ten aliiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE jana kwa simu kutoka Mbeya kwamba, moja ya vipaji vya kujivunia kwenye timu kwa sasa ni makipa wake vijana.
    Ten aliwataja makipa hao waliopandishwa kutoka timu ya vijana ya Mbeya City ni Fikirini Bakari, Hamisi Mchabila na Nurdin Mohammed.
    Kipa namba moja wa Mbeya City, Mmalawi, Owen Chaima amedaka mechi zote 15 za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kufungwa mabao 15

    “Kwa kweli hawa vijana wote wanafanya vizuri mazoezini na hata benchi la ufundi linavutiwa nao. Ni matumaini yetu kama wataendelea na juhudi hizi, watakuwa makipa bora baadaye,”alisema Ten.
    Kipa namba moja wa Mbeya City kwa sasa ni Mmalawi, Owen Chaima aliyedaka mechi zote za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Mlinda mlango huyo aliye katika msimu wake wa kwanza Mbeya, alidaka mechi 15 za Ligi Kuu na kufungwa mabao 15.
    Mechi ambayo alionyesha kiwango kikubwa zaidi ni dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC Novemba 2 mwaka huu Mbeya City wakishinda 2-1 Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
    Na haikushangaza baada ya mzunguko wa kwanza, Chiama aliyetokea klabu ya kwao Malawi akatajwa kuwaniwa na vigogo wa soka nchini, Simba SC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY YAJIVUNIA MAKIPA WAKE WADOGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top