• HABARI MPYA

    Sunday, October 02, 2016

    SERENGETI BOYS YATOLEWA NA KONGO FAINALI ZA VIJANA AFRIKA

    Na Mwandishi Wetu, BRAZZAVILLE
    TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imeshindwa kukata tiketi ya Fainali za Afrika mwakani Madagascar baada ya kufungwa 1-0 na wenyeji Kongo - Brazzaville jioni jii Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Debat mjini Brazaville katika mchezo wa marudiano hatua ya mwisho ya mchujo.  
    Kwa matokeo hayo, Serengeti Boys inatolewa kwa bao la ugenini baada ya sare ya jumla ya 3-3, kufuatia kushinda 3-2 katika mechi ya kwanza wiki mbili zilizopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Wachezaji wa Serengeti Boys iliyo chini Mkurugenzi wa Ufundi, Mdenmark Kim Poulsen, Kocha Mkuu, Bakari Shime na Kocha wa makipa na Muharami Mohammed ‘Shilton’ wapo kwenye huzuni kubwa baada ya matokeo hayo mjini Brazzaville.
    Hii inakuwa mara ya pili Serengeti Boys kuikosa kosa tiketi ya fainali za Afrika baada ya mwaka 2005 kufuzu fainali za Gambia, kwa kuzitoa Rwanda, Zambia na Zimbabawe, lakini ikaenguliwa kwa kashfa ya kumtumia mchezaji aliyezidi umri, Nurdin Bakari aliyekuwa anachezea Simba SC wakati huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERENGETI BOYS YATOLEWA NA KONGO FAINALI ZA VIJANA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top