• HABARI MPYA

  Friday, October 21, 2016

  PLUIJM AJA NA 'PLAN B' YANGA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm amesema kwamba ataendelea kubadilisha badilisha wachezaji katika mechi zijazo ili kuwapa nafasi ya kupumzika baina yao.
  Akizungumza jana kwa simu kutoka Mwanza, Pluijm alisema kwamba baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Toto Africans, sasa anaelekeza nguvu zake katika mchezo ujao dhidi ya Kagera Sugar Jumamosi mjini Bukoba.
  Na amesema kwamba timu yake jana ilicheza vizuri kwa kuwa kuna baadhi ya wachezaji aliwatumia baada ya mapumziko ya muda mrefu. “Oscar Joshua, Hassan Kessy na Haruna Niyonzima wote wamepata mapumziko ya kutosha na jana (juzi) walicheza vizuri  kwa sababu walikuwa wana hamu ya kucheza,”alisema.
  Pluijm amesema kwamba ataendelea kubadilisha badilisha wachezaji katika mechi zijazo ili kuwapa nafasi ya kupumzika baina yao

  Pluijm alisema kwamba ataendelea na mpango huo wa kubadilisha badilisha wachezaji ili kuwapa wote nafasi za kucheza na kupumzika. 
  Yanga SC juzi ilijiimarisha kidogo kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
  Kwa ushindi huo uliotokana na mabao ya Mzambia Obrey Chirwa na mzawa Simon Msuva, Yanga inafikisha pointi 18 baada ya kucheza mechi tisa ingawa inaendelea kukamata nafasi ya tatu, nyuma ya Stand United na Simba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PLUIJM AJA NA 'PLAN B' YANGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top