Mshambuliaji mpya wa Simba SC kutoka Ivory Coast, Frederick Blagnon (kushoto) aliyesajiliwa kwa dau la Sh. Milioni 100 akiwa ameketi benchi Jumamosi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu, Yanga ambao ulimalizika kwa sare ya 1-1. Blagnon pamoja na kuwa mchezaji ghali Simba, ameshindwa kumshawishi kocha Mcameroon Joseph Marius Omog kumpa nafasi kwenye kikosi cha kwanza
Kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga, Obrey Chirwa (kushoto) akiwa ameketi na Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' kwenye benchi wakati wa mchezo dhidi ya Simba Jumamosi. Chirwa aliyesajiliwa kwa dau la Sh. Milioni 200 ameshindwa kumvutia kocha Mholanzi wa Yanga, Hans van der Pluijm kumpa nafasi kwenye kikosi cha kwanza

0 comments:
Post a Comment