• HABARI MPYA

    Tuesday, August 05, 2014

    BOBBY WILLIAMSON KOCHA MPYA STARS

    Na Mwandishi Wetu, NAIROBI
    KOCHA wa Gor Mahia, Bobby Williamson amateuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars na anatakiwa kuanza kazi mara moja.
    Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF), Sam Nyamweya amethibitisha uteuzi wa kocha huyo wa zamani wa Uganda, Cranes katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo Nairobi Hotel. 
    Wanasoka wa zamani wa kimataifa wa Kenya, Mussa Otieno na Simon Mulama pia wameteuliwa kuwa Wasaidizi wa kocha huyo na Meneja.
    Mzoefu Afrika Mashariki; Bobby Williamson alifanya vizuri akiwa na Uganda na sasa anahamishia mafanikio hayo Kenya

    Jukumu la kwanza la Mscotland huyo litakuwa ni kutetea Kombe la Mataifa ya Afrika Mashaiki na Kati, CECAFA Challenge Novemba mwaka huu.
    Kocha huyo aliingia Afrika Mashariki Agosti mwaka 2008 alipopewa jukumu la kuifundisha Uganda Cranes ambako alidumu kwa miaka mitano kabla ya kuhamia Gor Mahia Julai 5 mwaka 2013.
    Bobby anachukua nafasi ya Adel Amrouche aliyefukuzwa baada ya Kenya kushindwa kuingia kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Morocco, kwa kutolewa na timu dhaifu, Lesotho. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BOBBY WILLIAMSON KOCHA MPYA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top