• HABARI MPYA

    Thursday, August 28, 2014

    TWIGA STARS KWENDA AFRIKA KUSINI IJUMAA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajia kuondoka nchini Ijumaa (Agosti 29 mwaka huu) kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya nchi hiyo (Banyana Banyana).
    Twiga Stars inakwenda huko kwa mwaliko wa Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA) kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Jumapili (Agosti 31 mwaka huu) katika mji wa Polokwane.

    Msafara wa timu hiyo utaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Saloum ambapo utajumuisha wachezaji 18 na benchi la ufundi lenye watu watano.
    Wachezaji kwenye msafara huo ni Amina Bilali, Anastaz Katunzi, Asha Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma, Etoe Mlenzi, Fatuma Jawadu, Fatuma Makusanya, Fatuma Maonya, Fatuma Swaleh, Happiness Mwaipaja, Maimuna Said, Mwajuma Abdillahi, Mwanahamis Shurua, Shelda Mafuru, Sophia Mwasikili, Therese Yona na Zena Rashid.
    Benchi la Ufundi linaongozwa na Kocha Rogasian Kaijage, na msaidizi wake Nasra Mohamed. Wengine ni Christine Luambano (daktari), Furaha Mnele (Meneja) na Mwanahamisi Nyomi (mtunza vifaa). Timu hiyo inatarajia kurejea nchini Septemba 2 mwaka huu kwa ndege ya Fastjet.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TWIGA STARS KWENDA AFRIKA KUSINI IJUMAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top