• HABARI MPYA

    Monday, August 25, 2014

    PAKA JEUSI LAKATIZA UWANJANI CAMP NOU, BARCA YAUA 3-0 LA LIGA

    BARCELONA imeanza vyema La Liga kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Elche Uwanja wa Camp Npu usiku wa kuamkia leo.
    Katika mchezo huo, kiungo wa Barca Javier Mascherano alitolewa nje kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza, kocha mpya Luis Enrique akiiongoza timu kwa mara ya kwanza, alionyesha mwanzo mzuri.
    Mambo hayo; Paka mweusi akikatiza Uwanja wa Camp Nou jana
    Mchezaji wa timu gani? Paka huyu alisababisha mechi isimame ili kwanza apite
    Lionel Messi kushoto akifurahia baada ya kufunga mabao mawili

    Lionel Messi aliifungia Barca bao la kwanza baada ya kuwazidi ujanja mabeki sita Elche, kabla ya kinda Munir El Hadaddi kufunga la pili, mabao yote kipindi cha kwanza. 
    Nyota wa Argentina, Lionel Messi alifunga bao lake la pili na la tatu la kuhitimisha ushindi wa Barca baada ya jitihada binafsi kipindi cha pili.
    Paka mweusi alikatiza Uwanja wa Camp Nou mwanzoni tu mwa mchezo na kusababisha mechi isimame kwa muda ili aondoke. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PAKA JEUSI LAKATIZA UWANJANI CAMP NOU, BARCA YAUA 3-0 LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top