• HABARI MPYA

    Sunday, August 24, 2014

    SIMBA SC YAIJIBU YANGA SC, YAUA 2-1 AMAAN USIKU HUU

    na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR
    KIUNGO Haroun Chanongo ametokea benchi na kuipa Simba SC ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kilimani City katika mchezo wa kirafiki usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
    Simba SC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa bao moja, lililofungwa kwa penalti na kiungo wake aliyerejea kikosini, Shaaban Kisiga ‘Malone’ dakika ya 14.
    Penalti hiyo ilifuatia kiungo Uhuru Suleiman kuangushwa kwenye eneo la hatari na beki wa Kilimani City, inayocheza Ligi Daraja la Pili wilaya Mjini, mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar, Rashid Ally.
    Beki Rashid Ally wa Kilimani City, akimchezea rafu Uhuru Suleiman kwenye eneo la hatari ambayo ilizaa penalti iliyoipa Simba SC bao la kwanza  

    Kipindi cha pili, kocha Phiri alibadilisha karibu kikosi kizima kilichoanza, kasoro Kisiga pekee.
    Kilimani ilisawazisha dakika ya 76 kupitia kwa Hassan Ameir aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Adam Abdallah baada ya kuwahadaa mabeki wa Simba SC. 
    Chanongo aliyeingia kipindi cha pili, aliisawazishia Simba SC zikiwa zimebaki dakika saba.
    Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Hussein Sharrif ‘Cassilas’, Nassor Masoud ‘Chollo’/Miraj Adam, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’/Said Ndemla, Hussein Butoyi/Joram Mgeveke, Uhuru Suleiman/Abdallah Seseme, Amri Kiemba/Haroun Chanongo, Amisi Tambwe/Elias Maguri, Shaaban Kisiga ‘Malone’ na Ramadhani Singano ‘Messi’/Abdi Banda. 
    Kilimani City; Hafidh Ally, Mzee Abdallah, Mzee Kheri, Kassim Omar, Mohammed Hajji, Lukman Ayoub, Abdulwahid Muhsin, Adam Abdallah/Hassan Shaame, Bakari Bakari, Rashid Ally na Matar Mohammed/Mashi Shehe. 
    Kikosi cha Simba SC kilichoanza
    Kocha Patrick Phiri na Msaidizi wake, Suleiman Matola kwenye benchi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAIJIBU YANGA SC, YAUA 2-1 AMAAN USIKU HUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top