• HABARI MPYA

    Sunday, August 24, 2014

    ALAN WANGA AIPA MERREIKH UBINGWA WA KAGAME, APR WANYAMAZISHWA NYUMBANI

    Na Nagma Khalid, KIGALI
    KLABU ya Merreikh ya Sudan imetwaaubingwa wa la Afrika Mashariki na Kati, Kombe la kagame jioni ya leo baada ya kuwafunga wenyeji, APR bao 1-0 Uwanja wa Amahoro, Kigali, Rwanda.
    Shukrani kwake, mfungaji wa bao hilo pekee mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Alan Wanga aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 24 akimalizia krosi ya Ragi Abdallah.
    Hilo linakuwa taji la michuano hiyo kwa Merreikh iliyoitoa Azam FC katika Robo Fainali kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 0-0, awali ikibeba taji mwaka 1986 na 1994.
    Kikosi cha Merreikh leo, Wanga wa katikati waliosimama

    Katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu uliotangulia leo, Polisi ya hapa iliifunga KCC ya Uganda kwa penalty 4-2 kufuatia sare ya 0-0.
    Kwa ushindi huo, El Merreikh wamezawadiwa dola za Kimarekani 30,000 wakati APR, imepata dola  20,000 kwa kushika nafasi ya pili wakayi Polisi iliyomaliza nafasi ya tatu imepata dola  10,000.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ALAN WANGA AIPA MERREIKH UBINGWA WA KAGAME, APR WANYAMAZISHWA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top