• HABARI MPYA

    Monday, August 25, 2014

    BALOTELLI ASAINI MIAKA MITATU LIVERPOOL, MSHAHARA MNONO NA JEZI NAMBA 45, AANZA KAZI LEO DHIDI YA MAN CITY

    MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 16 kutoka AC Milan kutua Liverpool kwa Mkataba wa miaka mitatau.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliwasili Melwood leo mchana kukamilisha uhamisho wake kabla ya kwenda kufanya mazoezi maalum na mkuu wa idara ya kuwaweka fiti wachezaji, Ryland Morgans. 
    Nyota huyo wa zamani wa Manchester City atakuwa akilipwa mshahara wa Pauni 125,000 kwa wiki Anfield na atakuwepo kwenye mchezo dhidi ya timu yake hiyo ya zamani usiku wa leo. Pamoja na kusaini mkataba wa miaka mitatu, Balotelli anaweza kuongezewa mwaka mmoja kwa mujibu wa kandarasi hiyo.
    Hakuna upweke: Mario Balotelli akiwa na jezi namba 45 Melwood baada ya kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 16 kutoka AC Milan
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BALOTELLI ASAINI MIAKA MITATU LIVERPOOL, MSHAHARA MNONO NA JEZI NAMBA 45, AANZA KAZI LEO DHIDI YA MAN CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top