• HABARI MPYA

    Thursday, August 28, 2014

    USAJILI LIGI KUU BARA WASOGEZWA MBELE TENA, SABABU YENYEWE NI ‘KICHEKESHO KWELI KWELI’

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    DIRISHA la usajili la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa wachezaji wazalendo limesogezwa mbele kwa Saa 48 kuanzia jana, kutokana na timu kushindwa kukamilisha usajili katika muda husika jana.
    Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, sababu za kusogeza mbele ni klabu zote za Ligi Kuu kushindwa kukamilisha usajili jana.
    “Nadhani wameshindwa kuutumia huu mfumo wetu mpya wa elektroniki, sasa tumewapa Saa 48 zaidi warekebishe, zikiisha hizo, hapo hakuna nafasi tena, tunasonga mbele,”amesema Mwesigwa.
    Yanga SC inatakiwa kuwa imekamilisha usajili wa Geilson Santana 'Jaja' hadi kufika Septemba 6, mwaka huu 

    Amesema kwamba hadi muda wa kufunga usajili jana Saa 6:00 usiku, ni timu moja tu, Kimondo FC ya Daraja la Kwanza ndiyo iliyokuwa imefanikiwa kukamilisha usajili wake katika mfumo huo. “Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Kimondo kwa kumudu kuutumia mfumo huu na kuwasilisha usajili wao ndani ya muda,”amesema. 
    Aidha, Mwesigwa amesema kwamba dirisha la usajili kwa wachezaji wa kigeni litafungwa Septemba 6, mwaka huu. “Hili dirisha la wachezaji wa kigeni likifungwa, hakuna nyongeza ya muda tena, kwa kuwa hili lipo katika mfumo wa kimataifa chini ya FIFA, likifungwa, limefungwa dunia nzima, hivyo nawasihi viongozi wa klabu wahakikishe hawafanyi makoasa,”amesema.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: USAJILI LIGI KUU BARA WASOGEZWA MBELE TENA, SABABU YENYEWE NI ‘KICHEKESHO KWELI KWELI’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top