• HABARI MPYA

    Thursday, March 20, 2014

    YANGA, SIMBA ZAPIGWA FAINI MILIONI 25

    Na Boniface Wambura, Dar es Salaam 
    KLABU za Yanga na Simba zimeagizwa kulipa jumla ya sh. Milioni 25 kutokana na uharibifu wa viti na vurugu zilizofanywa na washabiki wao kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly ya Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Yanga italipa sh. milioni 15 ambayo ni gharama ya uharibifu wa viti uliofanywa na washabiki kwenye mechi hiyo. Pia imepigwa faini ya sh. milioni tano kutokana na vurugu za washabiki wake. Nayo Simba imepigwa faini ya sh. milioni tano kutokana na washabiki wake kuhusika katika vurugu hizo.

    Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha dharura kilichofanyika jana (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
    TFF imetoa onyo kwa washabiki wa mpira wa miguu kujiepusha na vurugu viwanjani ikiwemo uharibifu wa miundombinu mbalimbali ya viwanja ikiwepo viti, na imeahidi kuchukua hatua kali zaidi kwa klabu na washabiki wake iwapo vitendo hivyo vitajitokeza tena.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA, SIMBA ZAPIGWA FAINI MILIONI 25 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top