• HABARI MPYA

    Friday, March 21, 2014

    KAMPUNI MPYA YA SIMU HIYOOOO TANZANIA

    “IPS kukuza ujasiliamali wa jamii katika mawasiliano ya simu Burundi, Uganda na Tanzania
    Machi 19, 2014 Shirika la kuhamasisha viwanda (IPS), chombo na silaha ya maendeleo ya viwanda chini ya mfuko wa maendeleo ya uchumi wa Aga Khan (AKFED) leo wanatangaza kuingia katika soko la mawasiliano la Afrika Mashariki chini ya kampuni iitwayo SMART. Jina la kampuni ni matokeo ya kura zilizopigwa Afrika Mashariki katika kampeni ya Uvumbuzi. Kuzinduliwa kwa kampuni hiyo kutaisaidia AKFED kukuza huduma zake za kibiashara kwa jamii katika nchi za Burundi, Tanzania na Uganda lengo kuu likiwa kuwekeza na kuwahudumia wateja.
    Mkurugenzi mkuu wa Smart Afrika Mashariki, Abdellatif Bouziani akiongea na waandihsi wa habari wakakti wa utambulisho wa jina la mtandao wa simu za mkononi “SMART” ambapo jina hilo limepatikana kupitia promosheni ya NO NAME iliyoendeshwa mwishonimwa mwaka 2013.
    Washindi wa promosheni ya no name wakiwa pamoja na menejimenti ya SMART ya Tanzania na Afrika Masahariki.
    Mkurugenzi mkuu wa Afrika Mashariki, Abdellatif Bouziani akimtambulisha mkuu wa masoko  wa Smart Afrika Mashariki, Brain Azemchapwakati wa utambulisho wa mtandao wa SMART


    Mtandao wa IPS una uwanda/uelewa mpana katika sekta ya mawasiliano. Ni washirika wakubwa wa Roshan shirika linaloongoza katika utoaji wa huduma za mawasiliano nchini Afghanistan na pia washirika muhimu katika shirika la Tcell linaloongoza katika kutoa huduma Tajikistan. IPS pia ni wawekezaji wakubwa na wa pekee waliowekeza SEACOM submarine cable venture in East Africa. Wakati umefika ambao ushirika wa IPS ndani ya SMART utaleta ushirikiano na kuweka record ya ushirikiano wa makampuni ya simu Nepal na Cambodia  na kuwafanya wawe waongozaji katika soko hili.
    Kuzinduliwa kwa SMART kutashirikisha uzoefu wa AKDEF katika kuwekeza kwa lengo la kuhamasisha ujasiliamali na ujenzi wa uchumi wa sauti ambao utatoa fursa nyingi za ajira na kuboresha maisha ya watu. Afrika Mashariki. AKFED imewekeza Serena Hotels, Diamond Trust Bank, Jubilee Insurance Group, National Media Group na katika maeneo mbalimbali ya uzalishaji na miundombinu kama vituo vya nguvu ya umeme vya Bujagali na Tsavo.
    “Kazi zetu katika mawasiliano kwa njia ya simu hasa Roshan-Asia ya kati ni kuboresha uwekezaji wa jamii katika miundombinu ya jamii, huduma za afya na elimu. Pia kutengeneza biashara yenye mafanikio katika soko ili tuweze kujitofautisha na washindani wengine, Tunatazamia kuwa uwekezaji katika kampuni dada ya AKDN utakua umeenea katika nchi za Burundi, Tanzania na Uganda kwa zaidi ya miaka 100” alisema Lutaf Kassam Meneja wa IPS
    SMART itaingia katika masoko haya ikiwa na dhamira ya embrance tamaduni za ndani ili kuboresha jamii wanakofanyia kazi.mfano mzuri wa dhamiri hii ni njia ambayo jina la kampuni lilivyochaguliwa. Kampeni ya Tupe Jina ilizinduliwa mwishoni mwa mwaka 2013 ikiwahamasisha watu wa Afrika Mashariki kupendekeza na kulipigia kura jina la kampuni. Kampeni hiyo iliwavutia zaidi ya watu 70,000 na majina tofautitofauti yalipendekezwa na kupigiwa kura. Mwisho kampeni ililipata jina la SMART ikikusudia kuangalia uvumbuzi wa mawazo katika soko la Afrika Mashariki.
    Kujifunza zaidi kuhusu SMART tembelea website yetu. Mawasiliano: Nicolous John, nicolousj.@bol.co.tz (+255 798 020 137).”
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAMPUNI MPYA YA SIMU HIYOOOO TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top