• HABARI MPYA

    Monday, March 31, 2014

    SERIKALI YAKUSANYA BILIONI 215 KWA NUSU MWAKA, NI KATIKA MPANGO WA BIG RESULTS NOW

    Na Mwandishi Wetu, Mlandizi 
    SERIKALI imekusanya jumla ya shilingi bilioni 215.0 katika kipindi cha Julai hadi Disemba, 2013 kutokana na hatua mpya za kodi zilizoibuliwa kwenye maabara za “Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa” yaani Big Results Now (BRN), utaratibu unaotumiwa na Serikali katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa baadhi ya majukumu yake kwa lengo la kupata matokeo makubwa kwa muda mfupi. 
    Haya yamo katika taarifa aliyoitoa msemaji mkuu wa wizara ya Fedha Ingiahedi Chediel Mduma alipokuwa akitoa taarifa ya utaratibu huo kwa wanablogu, katika kikao maalum na wadau hao kilichofanyika nje kidogo ya mkoa wa Pwani, maeneo ya Misugusugu, Mlandizi.
    Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Chediel Mduma akizungumza na wanablogu katika semina iliyofanyika Misugusugu, Mlandizi mkoani Pwani mwishoni mwa wiki
    Mtendaji Mkuu wa BIN ZUBEIRY Blog, Mahmoud Zubeiry kushoto alikuwepo
    Mdau kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Muhiddin Sufiani ambaye pia anamiliki blogu ya Sufiani Mafoto naye alihudhuria

    Bi Mduma alisema Wizara ya Fedha ni miongoni mwa Sekta zinazotekeleza utaratibu huu hususan katika eneo la utafutaji wa mapato (Resource mobilization), sekta nyingine ni Elimu, Kilimo, Maji, Uchukuzi na Nishati.  
    Utekelezaji wa kila sekta unazingatia viashiria vilivyoibuliwa katika uchambuzi wa kimaabara ulioratibiwa na Serikali kwa kushirikiana na wataalam kutoka nchini Malaysia. 
    Alisema huu unaiwezesha Serikali kuongeza ufanisi katika kusimamia utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo usimamiaji wa miradi kwa kuweka wazi malengo yaliyokusudiwa pamoja na kuainisha  viashiria vya utekelezaji ili kuongeza uwajibikaji kwa kila mshiriki.  Aidha, viashiria hivi hutumika kupima hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa maeneo ya kipaumbele na hivyo kuweza kupima mafanikio yaliyopatikana. Kadhalika, utaratibu huu unasaidia kurekebisha mapungufu katika utekelezaji kwa kuchukua hatua mapema na hivyo kuwezesha upatikanaji wa matokeo makubwa kwa haraka. 
    Bi Mduma amesema wizara yake imedhamirisa utafuta mapato ya ziada kiasi cha shilingi trilioni 3.8 hadi kufikia mwaka 2015/16;
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERIKALI YAKUSANYA BILIONI 215 KWA NUSU MWAKA, NI KATIKA MPANGO WA BIG RESULTS NOW Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top