• HABARI MPYA

    Thursday, March 20, 2014

    MCHEZAJI MAN UNITED ASEMA MOYES ASIPOFUKUZWA YEYE ANAONDOKA

    WAKALA wa kinda wa Manchester United, Marnick Vermijl amesema kwamba mteja wake atapenda kubakia Old Trafford iwapo tu kocha David Moyes ataondoka.
    Beki wa pembeni Mbelgiji, Marnick Vermijl mwenye umri wa miaka 22, amechezea mara kadhaa kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21 cha timu yake ya taifa na kwa sasa yupo kwa mkopo NEC Nijmegen msimu huu.
    Akizungumza na Hets Nieuwsblad, wakala wa Vermijl aitwaye Tony Dullers amesema: "Yupo ndani ya mkataba na Manchester United hadi Juni 2015, lakini zaidi itategemea na mazingira ya David Moyes.
    Dili la muda mfupi: Vermijl ameruhusiwa kucheza kwa mkopo NEC ya Uholanzi msimu huu
    Youth product: The Belgian arrived at Manchester United from Standard Liege in 2010
    Youth product: The Belgian arrived at Manchester United from Standard Liege in 2010
    Zao la uzalishaji vijana: Mbelgiji huyo alitua Manchester United akitokea Standard Liege mwaka 2010
     
    "Ikiwa kocha atabaki, kisha haitaonekana vizuri, kwa sababu alimuacha Marnick aende kwa urahisi NEC. Ikiwa Moyes atafukuzwa, inaweza kufungua nafasi kubwa (ndani ya United).
    "Kwa Manchester United, wanafurahia sana maendeleo yake. Wanataka Marnick afanye kazi katika klabu bora msimu ujao, lakini si kutolewa kwa mkopo tena. Aidha anaweza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza, au kuuzwa moja kwa moja,".
    Dullers amesema kwamba Ajax na klabu nyingine kadhaa za Ligi Kuu Engand zimeonyesha nia ya kumsajili beki huyo, wakati atakutana pia na Genk na Anderlecht wiki zijazo.
    International duty: The United man has seven caps for Belgian Under 21s
    Majukumu ya kimataifa: Mchezaji huyo wa Man United ameichezea mechi kadhaa U21 ya Ubelgiji
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MCHEZAJI MAN UNITED ASEMA MOYES ASIPOFUKUZWA YEYE ANAONDOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top