• HABARI MPYA

    Saturday, March 22, 2014

    ROONEY APIGA BAO LA KIHISTORIA MAN UNITED IKING'ARA ENGLAND

    MSHAMBULIAJI Wayne Rooney usiku huu amekumbushia enzi za David Beckham alipoifungia bao la umbali wa mita 58 Manchester United ikiifunga West Ham mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Upton Park.
    Akirejea katika Ligi Kuu baada ya kufanikiwa kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuitoa Olympiacos ya Ugiriki, mwanasoka huyo wa kimataifa wa England aliifungia mabao mawili timu ya David Moyes dakika ya nane na 73 na kuiwezesha kubeba pointi tatu.
    Bao la pili la Rooney limemfanya atimize mabao 212 na kumfikia Jack Rowley katika nafasi ya tatu ya ufungaji bora wa kihistoria Man United, lakini ni bao lake la kwanza alilofunga dakika ya nane ambalo litabakia katika kumbukumbu.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alifunga bao la ajabu, akikumbushia bao alilofunga Beckham dhidi ya Wimbledon mwaka 1996. United sasa inatimiza pointi 51 baada ya mechi 30, ingawa inabaki nafasi ya saba, ikizidiwa pointi mbili na Tottenham Hotspur iliyo nafasi ya sita.
    Bao ambalo halitasahaulika: Rooney amefunga bao kutoka umbali wa mita 57.9 Uwanja wa Upton Park usiku huuUnbelievable: Wayne Rooney scores from just inside West Ham's half after seven minutes
    Wayne Rooney baada ya kufutumua shuti la mbaliSpectacular: United team-mate celebrate the opening goal with Rooney in the early stages
    Pongezi: Wachezaji wa United wakimpongeza Rooney baada ya bao la kwanza
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ROONEY APIGA BAO LA KIHISTORIA MAN UNITED IKING'ARA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top