MSHAMBULIAJI Lionel Messi jana aliugua Uwanja wa Taifa wa Bucharest wakati Argentina ikilazimishwa sare ya bila kufungana na Romania.
Mshambuliaji huyo wa Barcelona alishindwa kuibomoa safu kali ya ulinzi ya Romania katika mchezo huo.
Messi aliuanza taratibu mchezo huo na ghafla akajiinamia uwanjani dakika ya saba muda mfupi baada ya kupiga mpira wa adhabu.
Baada ya mechi, Messi akasema juu ya maradhi yake: "Hii ni hali ambayo wakati wote inanitokea, imetokea mara chache nikiwa na Barça. Si kitu kwangu,".

Messi uwanjani jana

Messi akipasua katikati ya wachezaji wa Romania, Aleksandru Bourceanu, Aleksandru Chipciu, Mihai Pintilii na Dragos Grigore

Messi akimtoka Mihai Pintilii (kulia) Uwanja wa Taifa jana

Messi akiruka juu dhidi ya beki wa zamani wa West Ham, Razvan Rat (kulia).



.png)
0 comments:
Post a Comment