• HABARI MPYA

    Sunday, January 19, 2020

    TATIZO KUBWA NCHINI NI WACHEZAJI WETU KUKOSA MISINGI YA SOKA

    Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
    NDIVYO unavyoweza kusema, na hili limekuwa likionekana mara nyingi sana,kwa asilimia 99 wachezaji wanaocheza kwenye ligi yetu hawana misingi bora ya mpira,wengi wametoka mtaani na kuja kucheza ligi,misingi hiyo ya mpira inapatikana kwenye shule zinazotoa mafunzo ya mpira yaani akademi.⚽
    Kwa wenzetu ambao wametuacha kidogo kimaendeleo kwenye soka,wana akademi za kutosha,mchezaji anatakiwa aanze kupata mafunzo ya soka akiwa na umri wa miaka 7,baadae akija kwenye soka la ushindani utakuta  makocha wanamfurahia,👏🏽👏🏽👏🏽anaweza kufanya anachoelekezwa na inatumika nguvu ndogo sana kumuelekeza jambo.
    ❓Kwa nini nasema yote haya,najaribu kuona namna ambavyo makocha wageni wanavyopata tabu na hizi timu zetu,wachezaji wanakuwa wazito mno kushika wanachofundishwa,hawatoi hata asilimia 25 ya kinachohitajika kwao.

    Utaona alivyokuja Venderbroek pale Simba alisita kuingiza vitu vipya kwa haraka,akawa bado anaishi kwenye kivuli cha Patrick Aussiems,na akawa anapata matokeo tena makubwa kwenye mechi zake tatu za mwanzo,alipojaribu kuingiza vitu vipya tu,Simba ikaanza kuonekana inacheza hovyo,wengine wanasema wachezaji hawana fitnes,kila mwenye mdomo aliongea la kwake,lakini ukweli ni kwamba wachezaji ni wazito mno kushika mafundisho ya walimu wao.👍👍
    Itazame Yanga,unadhani wanakosa nini,wana kila mchezaji anayeweza kuisaidia timu kupata matokeo,lakini ukweli ni kwamba wanahitaji muda kuzoea mtindo mpya wa kiuchezaji ambao kocha wao amekuja nao,kila kocha ana falsafa yake,na hakuna anayeweza kuishi kwenye falsafa ya kocha  aliyeondoka,misingi mibovu ya mpira waliyonayo wachezaji wetu ndio changamoto kwa makocha.
    Mchezaji mwenye misingi ya soka hasumbuliwi na vitu vidogo kama kubadilika kwa mfumo,mbinu. Unaweza kumtumia unavyotaka wewe na akakupa unachotaka,mifano ipo,utaona kwa wenzetu anakuja kocha mpya timu ilikuwa haipati matokeo, inaanza kupata tena kwenye mechi ya kwanza tu.Hiyo inakuonyesha maana halisi ya profesional player na local player,mchezaji akitoka Kenya,Uganda,Burundi na kuja kwenye ligi yetu wala haimaanishi kuwa anaweza kuwa profesional player,anawezaje wakati misingi ya mpira hana? kama atatumia zaidi ya siku 30 kushika mafundisho ya mwalimu basi hakuna shaka yoyote huyo ni local playe,hana tofauti na wachezaji wetu wa ndani ambao pengine wanaweza kuwa bora kuliko wao,na hao ndio wamejaa mno kwenye ligi yetu.

    (Dominick Salamba ni mchambuzi wa soka anapatikana pia kupitia katika Akaunti zake za instagram na Twitter. Tembelea: Twitter: @dominicksalamb1 na Instagram: @dominicksalamba. waweza pia kuwasiliana naye kwa simu namba +255 713 942 770) 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TATIZO KUBWA NCHINI NI WACHEZAJI WETU KUKOSA MISINGI YA SOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top