• HABARI MPYA

    Saturday, January 25, 2020

    'SERENGETI GIRLS' YASONGA MBELE KUFUZU KOMBE LA DUNIA U7 WANAWAKE BAADA YA KUICHAPA TENA BURUNDI 1-0 BUJUMBURA

    Timu ya taifa ya wasichana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 imefanikiwa kusonga mbele katika mchujo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2020 nchini India baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Burundi bao pekee la Protasia Mbunda leo Uwanja wa Intwari mjini Bujumbura.
    Tanzania 'Serengeti Girls' wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 6-1 baada ya kushinda 5-1 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam Januari 12 na sasa watamenyana na mshindi wa jumla kati ya Uganda na Ethiopia zitakazorudiana kesho Bahir Dar. Mechi ya kwanza Uganda ilishinda 2-0 Januari 11 Jijini Kampala
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: 'SERENGETI GIRLS' YASONGA MBELE KUFUZU KOMBE LA DUNIA U7 WANAWAKE BAADA YA KUICHAPA TENA BURUNDI 1-0 BUJUMBURA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top