• HABARI MPYA

  Friday, November 02, 2018

  YANGA WASISTIZA MWENYEKITI WAO BADO MANJI TU NA WANASUBIRI BARUA YA BMT WAANZE MCHAKATO WA UCHAGUZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIKU moja baada Baraza la Michezo la Taifa (BMT), kuitaka klabu ya Yanga kufanya uchaguzi klabu hiyo imesema bado inamtambua Yussuf Manji ni Mwenyekiti wao.
  BMT jana iliiwataka Yanga kuitisha uchaguzi wake kwa ajili ya kujaza nafasi za viongozi waliojizuru huku ikiwemo ya Manji aliyeiandika barua ya kujiuzuru hivi karibuni.
  Taarifa ya BMT kwa vyombo vya Habari ilisema kwamba, Yanga imebaki na Wajumbe wanne kati ya 13 waliochaguliwa katika uchaguzi wa Juni 12, mwaka 2016 Dar es Salaam.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten wanasubiria kuletewa barua kutoka BMT ndio waanze mchakato wa uchaguzi. 

  Yanga imeendelea kusistiza inamtambua Yussuf Manji ndiye Mwenyekiti wake tu

  Ten alisema, hawana taarifa yeyote yeyote ya wao kufanya uchaguzi ila kama wataletewa barua basi watalifanyia kazi suala hilo. 
  “Sipendi kulizungumzia kwa urefu suala la uchaguzi hivi sasa ila wanachama wetu napenda kuwajuza kuwa hadi kufikiwa leo hatujapokea barua yeyote inayotutaka kufanya uchaguzi na kama tutapata basi tutaanza mchakato huo mara moja, " alisema Ten. 
  Ten alisema kuwa kulizungumzia hilo mara baada ya kupokea barua kutoka “BMT na Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF).
  Klabu ya Yanga imekuwa ikiahirisha mara kwa mara kufanya uchaguzi wake, licha ya Juni 10 mwaka huu Waziri Mwakyembe kuwataka wafanye uchaguzi kuziba mapengo ambayo yapo wazi.
  Kati ya viongozi wa klabu hiyo ambao waliingia madarakani Julai mwaka juzi, viongozi sita wamejiuzulu nafasi hizo wakidai kuwa na majukumu mengi.
  Viongozi waliojiuzulu ndani ya klabu hiyo ni Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga, na wajumbe Hashimu Abdallah, Salum Nkemi, Omary Said, Ayoub Nyenzi na huku waliobaki ni wajumbe Thobias Lingalangala, Samwel Lukumay, Siza Lyimo na Hussein Nyika. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA WASISTIZA MWENYEKITI WAO BADO MANJI TU NA WANASUBIRI BARUA YA BMT WAANZE MCHAKATO WA UCHAGUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top