• HABARI MPYA

    Sunday, November 18, 2018

    AZAM AKADEMI YASHIRIKI MICHUANO YA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 17 INAYOANZA LEO UWANJA WA KARUME

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya vijana ya Azam chini ya umri wa miaka 17 (Azam FC U-17) inashiriki michuano ya Kombe la Fasdo inayotarajiwa kuanza leo kwenye Uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam.
    Azam U-17 itafungua dimba na Sniper FC Academy, mchezo unaotarajia kufanyika kesho Jumamosi saa 10 jioni.
    Michuano hiyo inayoshirikisha timu 16 za wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam zenye vikosi vya vijana chini ya umri wa miaka 17, itakuwa na timu mbili za vijana kutoka vikosi vya Ligi Kuu, mbali na Azam FC nyingine ni African Lyon.
    Miongoni mwa timu 16 shiriki, waandaaji wamezigawa katika makundi manne yenye timu nne kila moja, ambapo timu mbili za juu za kila kundi zinatarajia kufuzu kwa robo fainali kabla ya mchezo wa nusu fainali na hatimaye fainali kufanyika.
    Kocha wa Azam Akademi (U-17), Idd Cheche (kushoto) anataka kutumia michuano hiyo kuwapa ushindani wachezaji wake

    Bingwa wa michuano hiyo anatarajia kubeba taji la kitita cha Sh. milioni mbili, mshindi wa pili atavuna Sh. milioni moja, mshindi wa tatu Sh. laki tano huku Mchezaji Bora na Mwamuzi Bora kila mmoja akitarajia kuchota Sh. laki mbili.
    Kocha wa timu ya Azam U-17, Idd Cheche, amesema kuwa malengo makuu ya kikosi chake kuingia kwenye michuano hiyo ni kuwapa ushindani wachezaji wake huku akieleza kuwa atakuwa akiangalia viwango vya wachezaji wake badala ya kuangalia matokeo zaidi.
    Alisema huo ni mwanzo tu kwa timu yake kuanza kushiriki michuano, akidai wamepanga ishiriki michuano mingi ya ndani ya nje ya nchi, ambapo mwezi ujao watashiriki kwa mara pili Chipukizi Cup mkoani Arusha huku wakiangalia uwezekano wa kushiriki mingine mikubwa nchini Afrika Kusini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM AKADEMI YASHIRIKI MICHUANO YA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 17 INAYOANZA LEO UWANJA WA KARUME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top