• HABARI MPYA

    Thursday, November 22, 2018

    KWANZA AMUNIKE, LAKINI PILI HATUKUJIANDAA KUSHINDANA

    Na Gharib Mzinga, DAR ES SALAAM
    Ni wazi kwamba Amunike ametuudhi watanzania hili wala halipingiki, Licha ya udhaifu wetu lakini ule mchezo ilikua dhaifu sana, Amefifisha Ndoto zetu za kwenda Afcon na kutuacha katika hesabu za vidole, kwamba tuifunge Uganda na pili tusubiri kusikia kama Mbabe wetu Lesotho kashindwa ndipo tufuzu. Anyway Amunike amelaumiwa sana na imestahili tuliache hili moja.
    Nipo hapa kuangalia upande wa pili na madhaifu yetu, Ebu nikuambie kitu, huwenda usiamini lakini chukua hii huu mpira wa miguu tunaopenda sana upo katika baadhi ya maeneo,  namaanisha kuna ukanda umekua na uwezo mkubwa kuliko mwengine, mfano Bara la ulaya kuna ukanda wa kusini ndiko kwenye mpira hasa kuanzia klabu mpaka timu za taifa huko kusini ndio kwenye Italy, France, Germany, Portugal, Belgium na Spain hawa ndio miamba ya soka ulaya, upande wa kaskazini kuna Norway, Sweden, Denmark, Iceland, Latvia n.k huku hakuna kitu.
    Bara la Amerika upande wa kusini ndiko kwenye mpira yaani Uruguay, Brazil, Chile, Argentina, Paraguay n.k lakini upande wa kaskazini (USA) hakuna kitu, ovyo kabisa. Na kwa hapa Afrika upande kwenye soka hasa ni Afrika Kaskazini Yani Misri, Morocco, Algeria, Tunisia na upande wa Magharibi yani  Nigeria, Senegal, Cameroon, Ivory coast, Ghana n.k 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Joseph Magufuli alitoa Sh. Milioni 50 kuchangai maandalizi ya Taifa Stars kabla ya mchezo na Lesotho

    Mataifa haya yana uhakika mkubwa wa kufuzu michuano mikubwa kama vile Afcon na WC, kama Miongoni mwa hayo mataifa moja wapo halijafuzu Afcon basi ni mshangao mkubwa ila yakifuzu sio story, ndio maisha yao ya kila Siku.

    Ukanda wa Afrika Mashariki na kusini huku Ardhi yetu haina rutuba ya Wachezaji bora, ambao wanaweza kuitikisa dunia kama Akina Didier Drogba, Samuel Etoo, El Hadji Diouf, George Weah, n.k hii inaonesha kwamba wenzetu wametuzidi pakubwa tu ndio maana wanatamba huko ulaya kwenye klabu kubwa kuliko Wachezaji wa ukanda wa Afrika mashariki na kusini waliopo huko.
    Unaweza ukadhani kwamba wenzetu wana Academy nyingi sana, na Miundombinu mikubwa  la hasha!!!! Nchi nyingi za kiafrika suala la Miundombinu zinafanana kwa asilimia kubwa, na laiti kama ingekua Miundombinu ndio sababu ya wao kutuzidi basi Afrika kusini lingekua taifa hatari zaidi barani Afrika.
    Issue ni kwamba wenzetu wana vipaji Vingi sana, na hii ni nature tu ya ukanda wao, hizo Academy zinaongeza tu ubora wao lakini tayari kuna vipaji lukuki. Sasa ili kufikia hapa walipo hawa wenzetu kuna jitihada kubwa ambazo nchi za kusini mwa Afrika inabidi zifanye.
    Kumbuka Miaka ya 1960, 1970 na 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990, Tanzania ilikuwa inafanana uwezo na mataifa mengi kisoka ukanda wa kusini mwa Afrika na Mashariki yake, ndio maana Taifa Stars iliweza kufika AFCON ya 1980 kwa kuitoa Zambia.
    Maisha yakaja kubadilika kwakua sisi hatuna vipaji vingi vya asili kwa miaka ya 90-2000's basi njia pekee ya kushindana na mataifa makubwa ni UWEKEZAJI MKUBWA.
    Mwandishi Mmoja wa vitabu vya Historia Aliyefahamika kwa Jina la Walter Rodney aliwahi kuandika "How Europe underdeveloped Africa" jinsi Bara la ulaya linakandamiza maendeleo ya Africa.
    Katika kitabu chake aliandika ivi 'kunako karne ya 15 ulaya na Afrika ilikua sawa kimaendeleo lakini kwa sasa kuna utofauti mkubwa, kuna Pengo kubwa lililotokea.
    Hii naileta na hapa kwenye soka letu mataifa mengi ya Kusini mwa Afrika yalikua yanafanana kiuwezo wa soka lakini Leo kuna pengo kubwa Miongoni mwao, kuna mataifa yamejizatiti kubadirika na yamefanikiwa kushindana na mataifa makubwa ki soka kwa muda mrefu, mafano. Zambia 2012 waliichapa Ivory coast ya Tembo Didier Drogba na mastaa kibao huku Zambia ikiwa na Wachezaji wa kawaida tu na wakabeba taji lao la kwanza.
    Zambia haikuenda kubaba Taji kwa bahati mbaya, Taifa hili lilishajijua kwamba uwezo wake duni hivyo likaamua kuwekeza haswa katika soka kwa kuanzisha vituo vya kulelea vijana, walileta wataalamu kutoka mataifa ya ulaya kama washauri na wakaanza kampeni za kuandaa walimu na vituo Konki kama vile Lusaka Youth Soccer Academy, Kabwe Youth Academy, Lusaka Celtics, Chiparamba Soccer Academy hizi ni Academy ambazo zinaandaa Wachezaji hodari zikiwa chini ya wataalamu wabobezi.
    Product ya vituo hivyo ni Lile taji la Afcon 2012.
    Pia wakaleta Kozi mbali mbali za walimu ili kuandaa walimu bora kisha wakapambana kupata mawakala ambao watatafuta soko kwa Wachezaji na walimu wao Ndiomaana kila ligi unayogusa Kusini mwa Afrika hukosi Wachezaji au walimu wazambia. Hili ni Gap kubwa sana.
    Taifa la  Zimbabwe lenyewe liliamua kuwekeza katika Vituo vichache ambavyo vinazalisha Wachezaji wenye ubora kupitia msaada wa mataifa ya ulaya mfano wa vituo hivyo ni Aces Youth Soccer Academy, Bantu Rovers FC, Friendly Academy, Highlanders FC Juniors.
    Congo na Uganda kwa sasa sio wenzetu sana kwani wamewekeza kwenye Mpira na kwa sasa wanaanza kuizoea michuano ya Mataifa Afrika, hawa pia hawakukurupuka, sisi watanzania tumeachwa tulipo huku tukiendelea na Siasa zetu za mpira, hatuna vituo vyenye tija, Walimu wazuri wala mawalaka kwaajili ya kutoa products zetu kwenda kushindana nje. Kwa hali hii tutaendelea kua wa kipekee huku Mauritania, na Madagascar wakituacha, kadri tunavyochelewa na Somalia watatupita pia.
    *SWALI* Asilimia kubwa ya Wachezaji wa stars ni Product ya kituo cha vijana cha Azam, Kaa uje na jibu la hili swali Je ? Hao Wachezaji wanasifa ya kuwaita Wachezaji wa kishindani kimataifa ? Gadiel Mbaga, Himid Mao, Abdala Kheri sebo, Aboubakar salum, Aishi Manula.
    *SWALI* Tuna walimu Wangapi wanaofundisha nje ya Tanzania ? 
    *SWALI* kuna mawakala wa Wachezaji wangapi unaowafahamu ? 
    Soka letu, kivyetuvyetu
    (Mwandishi wa makala haya, Gharib Mzinga ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kitivo cha Uandishi wa Habari, SJMC),
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KWANZA AMUNIKE, LAKINI PILI HATUKUJIANDAA KUSHINDANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top