• HABARI MPYA

  Saturday, November 03, 2018

  AL AHLY WAICHAPA ESPERANCE 3-1 FAINALI LIGI YA MABINGWA

  TIMU ya Al Ahly ya Misri jana imetumia vyema nafasi ya kucheza nyumbani, baada ya kuichapa mabao 3-1 Esperance ya Tunisia katika fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.
  Kwa ushindi huo, Ahly ni kama wameweka mkono mmoja kwenye taji la tisa la rekodi la Ligi ya Mabingwa Afrika, kwani sasa watahitaji sare au kufungwa kwa tofauti ya bao moja tu katika mchezo wa marudiano Novemba 9 mjini Tunis ili kutwaa tena Kombe hilo.
  Walid Soliman alifunga mabao mawili dakika za 34 na 76 na lingine Amr El Sulya dakika ya 58 upande wa Mashetani Wekundu wa Cairo, wakati bao pekee la Esperance lilifungwa na Youcef Belaili dakika ya 64.
  Esperance watahitaji ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa marudiano Ijumaa ijayo Uwanja wa Olimpiki mjini Rades kutwaa taji hilo.
  Kikosi cha Al Ahly kilikuwa; El Shenawy, Fathi/El Demerdash dk22, Samir, Coulibaly, Ashraf, Ashour, El Sulya, Hamoudi/Hussein dk67, Soliman, Mohareb na Azaro.
  Esperance; Cherifia; Dhaouadi, Badri, Belaili, Chemmam, Coulibaly, Derbali, Chaalali, Erbeia, Khenissi/Mejri dk79 na Kom.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AL AHLY WAICHAPA ESPERANCE 3-1 FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top