• HABARI MPYA

    Friday, November 23, 2018

    MCHUJO WA AWALI WA WAGOMBEA UONGOZI YANGA SC KUELEKEA UCHAGUZI WA JANUARI 13 WAFANYIKA LEO TFF

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MCHUJO wa awali wa wagombea uongozi wa klabu ya Yanga SC kuelekea uchaguzi wa Januari 13, mwakani unafanyika leo.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Malangwe Mchungahela ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo mjini Dar es Salaam kwamba kwamba zoezi la kupitia majina ya wagombea linafanyika leo.
    Mchungahela aliyechukua nafasi ya Wakili Revocatus Kuuli aliyefungiwa maisha kujihusisha na soka kwa kuvujisha siri za TFF, amesema kesho watatoa orodha ya wagombea waliopitishwa baada ya mchujo huo. 
    Baada ya hapo, zoezi litakalofuata ni Kamati ya Uchaguzi kupokea mapingamizi juu ya wagombea hadi Novemba 25 na kuyapitia na kuwafanyia usaili wagombea hadi Novemba 28.

    Mchungahela amesema kwamba Novemba 29 Kamati itatangaza matokeo ya usaili na kutaja orodha ya mwisho ya wagombea waliopitishwa, kabla ya kupelekea masuala ya Kimaadili kwa Sekretarieti ya TFF, ambayo itayawasilisha Kamati ya Maadili.
    Desemba 11 hadi 14 Kamati ya Maadili itatangaza uamuzi wa masuala ya Kimaadili iliyoyajadili, kabla ya kutoa fursa ya wagombea walioathirika na zoezi hilo kukata Rufaa na Januari 4 hadi 6 orodha kamili ya mwisho ya wagombea itatolewa baada ya michakato yote tayari kwa kampeni kati ya Januari 8 na 12.
    Wagombea Uenyekiti ni Dk. Jonas Benedict Tiboroha, Mbaraka Hussein Igangula, Erick A Ninga na Yono Kevela anayewania pia Umakamu pamoja na Titus Eliakim Osoro na Salum Magege Chota.
    Wanaowania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji pamoja na ni Hamad Ally Islam, Benjamin Jakcso Mwakasonda, Sylvestre Haule, Salim Seif, Mussa Katabaro, Shiftu Amri, Said Baraka, Pindu Luhoyo na Dominick Francis.
    Wengine ni Seko Jihadhari, Ally Omar Msigwa, Arafat Ally Hajji, Geoffrey Boniface Mwita, Frank Kalokola, Ramadhani Said, Leonard Marango, Bernard Faustin Mabula, Christopher Kashiririka, Athanas Peter Kazige na Justin Peter Bisangwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MCHUJO WA AWALI WA WAGOMBEA UONGOZI YANGA SC KUELEKEA UCHAGUZI WA JANUARI 13 WAFANYIKA LEO TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top