• HABARI MPYA

  Friday, November 02, 2018

  TFF YAMPANDISHA KAMATI YA MAADILI ALIYEKUWA MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI, WAKILI KUULI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limempeleka Kamati ya Maadili aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati yake ya Uchaguzi, Wakili Revocatus Kuuli kwa tuhuma za kuweka hadharani nyaraka za shirikisho hilo na kuzisambaza kwa watu wasiohusika.
  Katika barua aliyotumiwa Wakili huyo Oktoba 29, mwaka huu kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Wakili Hamidu Mbwezeleni, Kuuli anatakiwa kufika kwenye kikao hicho kesho kujieleza juu ya tuhuma zake.
  Shitaka la kwanza la Kuuli ni kusambaza barua za TFF kinyume cha kufungu cha 16 (1) cha kanuni za Maadili za TFF tole la mwaka 2013 kinyume cha ibara ya 12.1 (b).

  Shitaka la pili ni kutoa maelezo yanayoonyesha  kuwa na mgongano wa maslahi kwa kuwapa watu wasiohusika kinume cha kifungu cha 16 (2) cha kanuni za Maadili  za TFF na kosa la tatu ni kufanya vitendo vinavyoshuhsa hadhi ya shirikisho kinyume cha ibara ya 50 (1).
  Na haya yote yanatokea wakati tayati TFF imefanya mabadiliko ya Kamati ya Uchaguzi, ikimuondoa  Kauuli na wenzake wote na kumteua Malangwe Ally kuwa Mwenyekiti mpya. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAMPANDISHA KAMATI YA MAADILI ALIYEKUWA MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI, WAKILI KUULI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top