• HABARI MPYA

  Friday, November 02, 2018

  AFRICAN LYON WAWAPIGA LIPULI 2-0, COASTAL UNION NAO ‘WAWAFANYIZIA’ STAND UNITED PALE PALE SHINYANGA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya African Lyon imetumia vizuri Uwanja wa nyumbani, Uhuru mjini Dar es Salaam baada ya kuichapa 2-0 Lipuli FC ya Iringa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo.
  Kwa ushindi huo uliotokana na mabao ya mkongwe Haruna Moshi Shaaban ‘Boban’ dakika ya 14 na Kassim Mdoe dakika ya 26, African Lyon inafikisha pointi 11 baada ya kucheza mechi 13 na kupanda hadi nafasi ya 11 kwenye Ligi Kuu ya timu 20.
  Lipuli FC ya kocha Suleiman Abdallah Matola, yenyewe inabaki na pointi zake 12 baada ya kucheza mechi 12 na itaendelea kukamata nafasi ya 12.

  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Coastal Union ya Tanga imewalaza wenyeji, Stand United mabao 2-1 Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
  Haukuwa ushindi mwepesi wa Coastal Union, kwani ilibidi watoke nyuma baada ya Bigirimana Blaise kutangulia kuwafungia Stand United dakika ya saba tu ya mchezo huo.
  Na Coastal Union inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani, Juma Mgunda ikazinduka na kipindi cha pili kwa mabao ya Khamis Kanduru dakika ya 67 na Ayoub Lyanga dakika ya 85 kuibuka na ushindi wa 2-1 Kambarage.
  Kwa ushindi huo,  ‘Wana Mangushi’ wanafikisha pointi 19 baada ya kucheza mechi 13 na wanapanda kwa nafasi moja hadi ya tisa, wakati Stand United ‘Chama la Wana’, wanabaki na pointi zao 14 baada ya kucheza mechi ya 13 leo, wakiendelea kushika nafasi ya 11. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AFRICAN LYON WAWAPIGA LIPULI 2-0, COASTAL UNION NAO ‘WAWAFANYIZIA’ STAND UNITED PALE PALE SHINYANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top