• HABARI MPYA

  Friday, November 02, 2018

  FOMU ZA UWAKALA WA WACHEZAJI ZAANZA KUTOLEWA, GHARAMA ZAKE NI DOLA 2,000 ZA KIMAREKANI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeanza kutoa fomu za Uwakala wa Wachezaji.
  Fomu hizo zinapatikana kwenye ofisi za TFF Karume,Ilala na kupitia kwenye tovuti ya TFF.
  Wakati wa kujaza fomu ili ikamilike ni lazima muombaji aambatanishe na ripoti ya Interpol ambayo itasaidia kufahamu taarifa zake mbalimbali.

  Ada ya Uwakala ni 2000 USD kwa miaka miwili na baada ya kumalizika muda kila unapoomba kuongeza muda utatakiwa kulipia ada ya 500 USD kwa mwaka.
  Mwisho wa maombi ni Disemba 30,2018 na fedha yote inalipiwa Benki kupitia namba ya Akaunti ambayo ipo kwenye fomu ya maombi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FOMU ZA UWAKALA WA WACHEZAJI ZAANZA KUTOLEWA, GHARAMA ZAKE NI DOLA 2,000 ZA KIMAREKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top