• HABARI MPYA

  Thursday, November 01, 2018

  MISS TANZANIA, QUEEN ELIZABETH AKABIDHIWA BENDERA KWENDA KUSHIRIKI MISS WORLD CHINA

  Na Nasra Omary, DAR ES SALAAM
  WAZIRI wa Habari Sanaa Utamaduni, na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, amemkabidhi Bendera ya Taifa Mshindi wa ‘Miss’ Tanzania 2018 Queen Elizabeth, kwa ajili ya kuipeperusha katika Mashindano ya kumsaka Mlimbwende wa Dunia.
  Queen Elizabeth atasafiri Novemba 8, mwaka huu kuelekea nchini China, ambapo Mashindano ya kumsaka Mlimbwende wa Dunia (Miss World) yatakayofanyika katika Mji wa Sanya, nchini humo.
  Akizungumza katika ghafla hiyo Dk. Mwakyembe alisema, utoaji wa Bendera hiyo ni deni kubwa kwa Mlimbwende huyo, kwani anapaswa kuitendea haki kwa kurudi na ushindi.

  “Nimekuwa na utaratibu wa kutoa Bendera kama deni kwa ninayemkabidhi kwani ni lazima uitendee haki hivyo, tunatarajia uwakilishaji mwema wa Taifa la Tanzania kwa Queen Elizabeth kurudi na ushundi nchini,” Alisema.
  Alisema pia Mashindano hayo yakawe chachu kwa Queen Elizabeth, kuitukuza lugha ya Kiswahili kama alama ya Tanzania ili iendelee kuwa miongoni mwa lugha zinazozungumzwa zaidi Duniani kama ilivyo sasa.
  Dk. Mwakyembe aliongeza kuwa, katika mashindano yajayo Serikali inatengeneza utaratibu wa kuwaajiri kumi bora ya washiriki wengine wa mashindano hayo, kama wahudumu wa Ndege katika Shirika la Ndege hapa nchini ATCL.
  Nae Queen Elizabeth alisema safari ya kushiriki Miss World ni ndoto yake ya muda mrefu hivyo anatarajia kuiwakilisha vyema  Tanzania.
  “Safari hii hatuendi kucheza, nawaaminisha Watanzania kuwa nitarudi na heshima kubwa nchini kama ambavyo nimeagizwa na Waziri mwenye dhamana pia naahidi kuwa balozi mzuri wa lugha ya Kiswahili huko niendako,” Alisema.
  Hadi sasa Chuo cha usafirishaji nchini (NIT), kimetoa nafasi tatu za masomo bure kwa miongoni mwa kumi bora ya walioshiriki mashindano ya Miss Tanzania mwaka huu.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MISS TANZANIA, QUEEN ELIZABETH AKABIDHIWA BENDERA KWENDA KUSHIRIKI MISS WORLD CHINA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top