• HABARI MPYA

  Thursday, November 01, 2018

  SIMBA SC YAWAASA WANACHAMA WAKE KUCHAGUA VIONGOZI WATAKAOLETA MATAJI ZAIDI MSIMBAZI

  Na Nasra Omary, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa Klabu ya Simba umewataka wanachama wake kuzingatia wanachagua viongozi ambao wataifanya Simba licha ya kujiendesha kiuchumi, lakini iweze kupigania makombe yenye hadhi ikiwemo klabu bingwa Afrika.
  Simba inatarajiwa kufanya mkutano mkuu wa kikatiba sambamba na uchaguzi mkuu, utakaofanyika Novemba 4, utakaofanyika katika kituo cha Mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere(JNICC), Dar es Salaam.
  Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, alisema kuwa wanachama wajue kuwa wanachama wajue kuwa timu yao kwa sasa ipo kwenye mfumo wa hisa hivyo wanatakiwa kuchagua viongozi ambao watahakikisha timu hiyo inapata makombe ya Klabu Bingwa Afrika.

  "Tunashukuru kwamba wagombea wote ambao wamejitokeza ni wale ambao wanajua weledi na maadili ya soka nchini pia wanauzoefu mkubwa kwenye uongozi wa  soka nchini.
  Pia wanafurahi kuona wagombea wao wakifanya kampenzi nzuri na hakuna mgombea yeyote hadi sasa aliyekamatwa kwa kashfa ya rushwa hiyo inajionesha kuwa uchaguzi utakuwa wa amani,"  alisema Manara
  Manara aliwataka wanachama wa Simba ambao hawajalipa ada waweze kulipa mapema ili waweze kujumuika kwenye mkutano na kupiga kura.
  Aliwataka wanachama wote waweze kuwahi kwani kuanzaia saa 2:00 asubuhi mkutano mkuu utaanza hadi saa 6:30 mchana,  7:30 utaanza uchaguzi mkuu kwa ajili ya kuchagua  viongozi wapya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAWAASA WANACHAMA WAKE KUCHAGUA VIONGOZI WATAKAOLETA MATAJI ZAIDI MSIMBAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top