• HABARI MPYA

    Saturday, November 03, 2018

    MECHI YA MAHASIMU WA UTURUKI, GALATASARY NA FENERBAHCE VURUGU TUPU HADI SARE 2-2

    MECHI ya mahasimu wa Jiji la Istanbul ilitawaliwa na vurugu jana huku kiungo wa Fenerbahce, Jailson akikimbizwa nje ya Uwanja baada ya kuifungia timu yake bao la kusawazisha katika sare ya 2-2 na mahasimu, Galatasaray.
    Wachezaji watatu walitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuhusika katika vurugu kwenye mchezo uliofanyika Uwanja wa Telekom Arena.
    Mabao ya Ryan Donk dakika ya 31 na Martin Linnes dakika ya 49 yaliwaweka mbele Galatasaray, kabla ya Fenerbahce kuzinduka kwa mabao ya Mathieu Valbuena dakika ya 66 kwa penalti na Jailson dakika ya 72 na mchezo kumalizika kwa sare ya 2-2.

    Mechi ya mahasimu wa Jiji la Istanbul, Fenerbahce na Galatasaray ilitawaliwa na vurugu jana

    Badou Ndiaye anayecheza kwa mkopo Galatasaray kutoka Stoke, mshambuliaji wa zamani wa Tottenham, Roberto Soldado anayecheza Fenerbahce kwa sasa na Jailson wote walitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kugombana.
    Chanzo cha vurugu hizo ni Jailson kwenda kuwazomea mashabiki wa wenyeji baada ya kufunga bao la kusawazisha kwa shuti la umbali wa mita 25. 
    Akawaonyesha ishata ya kuudhi wenyeji baada ya mchezo na wachezaji wa Galatasaray wakamvaa kumpa kichapo kiungo huyo Mbrazil.
    Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 akaamua kujitoa kwenye na kukimbilia kwenye vyumba vya kubadilisjia nguo, lakini wachezaji Galatasaray walimfuata na kuendelea kumuadhibu.
    Kuna picha zinamuonyesha Ndiaye, ambaye aliteremka daraja hadi Championship akiwa na Potters msimu uliopita akimkaba Jailson Siqueira wa Fenerbahce kabla hajaonyeshwa kadi nyekundu.   
    Soldado, ambaye amecheza mechi nane bila kufunga msimu huu, pia alihusika kwenye vurugu hizo na alionekana akiwa amemkaba shingo Younes Belhanda.
    Beki wa zamani wa Liverpool, Martin Skrtel naye pia alihusika kwa kugombana na mwanasoka wa kimataifa wa Morocco, Belhanda.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MECHI YA MAHASIMU WA UTURUKI, GALATASARY NA FENERBAHCE VURUGU TUPU HADI SARE 2-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top