• HABARI MPYA

  Friday, November 02, 2018

  REFA MTANZANIA JONESIA RUKYAA KUCHEZESHA AFCON YA WANAWAKE NCHINI GHANA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  REFA wa Tanzania Jonesia Rukyaa amechaguliwa kuchezesha Fainali za Afrika za Wanawake zitakazofanyika nchini Ghana.
  Rukya amechaguliwa katika orodha ya Waamuzi wa katikati akiwa ni Mtanzania pekee katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Novemba 17 hadi Desemba 1, 2018.
  Jumla ya Waamuzi wa katikati 13 wamechaguliwa na Waamuzi wasaidizi 12.

  Jeonesia Rukyaa amechaguliwa kuchezesha Fainali za Afrika za Wanawake zitakazofanyika nchini Ghana

  Fainali hizo pia zitatumika kupata timu zitakazowakilisha Afrika kwenye Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake zitakazofanyika mwakani nchini Ufaransa.
  Washindi Watatu wa juu ndio watafuzu kucheza Kombe la Dunia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REFA MTANZANIA JONESIA RUKYAA KUCHEZESHA AFCON YA WANAWAKE NCHINI GHANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top