• HABARI MPYA

  Tuesday, November 21, 2017

  WILDER AMCHOKOZA TENA JOSHUA AKISISTIZA PAMBANO LA KUUNGANISHA MATAJI

  BONDIA Deontay Wilder ameendelea kumchokoza Muingereza, Anthony Joshua ili akubali pambano la kuunganisha mikanda ya uzito wa juu duniani. 
  Akitoka kumdunda kwa Knockout (KO) raundi ya kwanza Bermane Stiverne, bingwa wa WBC, Wilder anataka kuvaana na mmiliki mataji ya WBA na IBF, Joshua. 
  Joshua amekwishaweka wazi kwamba anayetaka kupigana naye afuate taratibu kwa kutoa ofa, ingawa mpinzani wake huyo, Mmarekani mwenye umri wa miaka 32 ameendelea kuomba pambano kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

  Deontay Wilder ameposti picha hii ameshika taji la WBC uzito wa juu leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA


  Wilder ametumia mtandao wa kijamii kumtia presha Joshua mwenye umri wa miaka 28 ambaye hajapoteza pambano kwa kuandika kwamba mkanda wake alioupa jina la utani, Sophia unapata upweke. 
  "Sophia anapata upweke,"amesema ameandika mbabe huyo kwenye ukurasa wake wa Twitter akiambatanisha na picha yake akiwa na mkanda wa WBC begani.
  "Anahitaji wake wenzake @anthony_joshua... usisubiri, panga tarehe MWENZANGU,"ameandiika.
  Wilder amethibitisha majadiliano ya pambano hilo yanaendelea na huenda kila bondia wote wakawa na pambano la kupasha kabla ya kukutana kwaop ulingoni.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WILDER AMCHOKOZA TENA JOSHUA AKISISTIZA PAMBANO LA KUUNGANISHA MATAJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top