• HABARI MPYA

  Wednesday, November 08, 2017

  KAMUSOKO NA TAMBWE KUREJEA DHIDI YA MBEYA CITY

  Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM
  DAKTARI wa Yanga, Edward Bavu amesema kwamba kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko na mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe wanaweza kurejea uwanjani wiki ijayo.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Bavu amesema kwamba wawili hao wameanza rasmi mazoezi wiki hii na kama wataendelea vizuri wanaeza kucheza mechi ijayo.  
  Yanga inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mbeya City Novemba 19, Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ikitoka kulazimisha sare ya 0-0 na Singida United Jumamosi iliyopita Uwanja wa Namfua, Singida.
  Na kuelekea mchezo huo, kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi chini ya makocha Wasaidizi, Mzambia Noel Mwandila, wazalendo Nsajigwa Shadrack na Juma Pondamali, baada ya kocha Mkuu, George Lwandamina kwenda kwao, Zambia kuhudhuria mazishi ya mpwa wake.  
  Lwandamima anatarajiwa kurejea nchini Jumanne wiki ijayo kuendelea na maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Sare dhidi ya Singida ilikuwa ya pili mfululizo baada ya Oktoba 28, mwaka huu pia kutoka 1-1 na mahasimu wao wa jadi, Simba.
  Yanga sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa na pointi 17 baada ya kucheza mechi tisa, nyuma ya Simba na Azam zenye pointi 19 kila moja baada ya mechi tisa pia.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAMUSOKO NA TAMBWE KUREJEA DHIDI YA MBEYA CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top