• HABARI MPYA

  Friday, March 17, 2017

  SAMATTA APELEKWA HISPANIA ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE

  DROO ya Robo Fainali ya UEFA Europa League imetoka leo na timu ya Nahodha wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta, KRC Genk ya Ubelgiji itamenyana na Celta Vigo ya Hispania.
  Mabingwa wa zamani wa Ulaya, Manchester United watamenyana na Anderlecht ya Ubelgiji, wakati Lyon ya Ufaransa itamenyana na Besiktas ya Uturuki na Ajax ya Uholanzi itavaana na Schalke ya Ujerumani.
  Mechi za kwanza zinatarajiwa kuchezwa Aprili 13 na marudiano Aprili 20, Manchester United na Genk wote wakianzia ugenini.
  Genk imefuzu Robo Fainali ya UEFA Europa League licha ya kulazimishwa sare ya 1-1 na KAA Gent usiku wa jana Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk, kwani ushindi wa 5-2 ugenini katika mchezo wa kwanza unawafanya wasonge mbele kwa ushindi wa jumla wa 6-3.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA APELEKWA HISPANIA ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top