• HABARI MPYA

  Friday, March 17, 2017

  NI REAL NA BAYERN, BARCA NA JUVE ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA

  MABINGWA wa England, Leicester City watamenyana na Atletico Madrid ya Hispania katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Watasafiri kwenda Hispania kumenyana na kikosi cha Diego Simeone kwenye mchezo wa kwanza Aprili 11 au 12 kabla ya kurudiana wiki moja baadaye England.  
  Mabingwa watetezi, Real Madrid ya Hispania watamenyana na Bayern Munich ya Ujerumani katika mchezo unaotarajiwa kuwa mkali zaidi kwenyen hatua hiyo, kikois cha Zinedine Zidane kikiwania kuwa timu ya kwanza kutetea taji hilo kwa mafanikio. 
  Barcelona ya Hispania itamenyana na Juventus ya Italia baada ya kufuzu kimiujiza Robo Fainali wakiwatoa Paris Saint-Germain, wakati Borussia Dortmund ya Ujerumani pia, itamenyana na Monaco ya Ufaransa. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI REAL NA BAYERN, BARCA NA JUVE ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top