Tovuti Hii hutembelewa na zaidi ya watu 60,000 kila siku, kutangaza biashara yako na www.binzubeiry.co.tz,
Tuma maombi kwa barua pepe 4thebetter@gmail.com.
 • HABARI MPYA

  Monday, March 27, 2017

  MECHI YA MBAO NA SIMBA YASOGEZWA MBELE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodaocm Tanzania Bara kati ya wenyeji Mbao FC na Simba SC ya Dar es Salaam uliokuwa ufanyike Aprili 8, mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza umesogezwa mbele kwa siku mbili hadi Aprili, 10.
  Taarifa ya Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura imesema kwamba hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha shughuli za kijamii kwenye Uwanja huo zitakazoanza Aprili 1 hadi 9.
  Simba SC inatarajiwa kuondoka Dar es Salaam katikati ya wiki kwenda mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa mechi zake za Ligi Kuu, ikianzia Bukoba itakapomenyana na Kagera Sugar Aprili 2, na baadaye Mbao FC Aprili 10 na kumalizia na Toto Africans Aprili 15. 
  Ikumbukwe Simba SC ndiyo inaongoza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa pointi zake 55 ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 53 baada ya timu zote kucheza mechi 24.
  Wakati Simba SC wakienda kucheza mechi za mwisho za ugenini mikoani, mahasimu wao Yanga watakuwa na michezo mfululizo ya nyumbani kuanzia Aprili 1 na Azam FC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Note: Only a member of this blog may post a comment.

  Item Reviewed: MECHI YA MBAO NA SIMBA YASOGEZWA MBELE Rating: 5 Reviewed By: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top