• HABARI MPYA

  Tuesday, October 04, 2016

  MECHI YA STARS NA WAHABESHI YAOTA MBAWA, VIJANA SASA KUPASHA TU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa kirafiki wa kimataifa kati ya wenyeji, Ethiopia na Tanzania uliokuwa ufanyike Jumamosi wiki hii umefutwa kutokana na vurugu zinazoendelea nchini humo.
  Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba, wametumiwa taarifa na wenyeji wao, Ethiopia wakisema kwamba mchezo huo hautakuwepo tena kwa sasa kwa sababu hali ya hewa si nzuri. 
  Na baada ya matokeo hayo, Mwesigwa amesema kwamba benchi la Ufundi chini ya Kocha Mkuu, Charles Boniface Mkwasa litaamua cha kufanya, lakini uwezekano wa kupata mchezo mwingine kwa muda huu ni mgumu.
  Wachezaji walioitwa katika kikosi cha Stars kwa ajili ya mchezo huo ni Makipa; Deogratius Munishi 'Dida' (Yanga SC), Said Kipao (JKT Ruvu) na Aishi Manula (Azam FC).
  Mabeki; Shomari Kapombe (Azam FC), Juma Abdul, Andrew Vincent, Mwinyi Hajji (Yanga SC), Mohamed Hussein 'Tshabalala' (Simba SC), David Mwantika (Azam FC) na James Josephat (Prisons).
  Viungo ni Himid Mao (Azam FC), Mohammed 'Mo' Ibrahim, 
  Jonas Mkude, Muzamil Yassin, Jamal Mnyate, Shiza Kichuya (Simba SC), Simon Msuva, Juma Mahadhi (Yanga SC) na Hassan Kabunda (Mwadui FC).
  Washambuliaji ni Ibrahim Hajib (Simba SC), John Bocco (Azam FC), Mbwana Samatta KRC Genk (Ubelgiji), Elius Maguli (Oman) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC). 
  Wachezaji wa nyumbani walianza mazoezi jana Uwanja wa Kituo cha Jakaya Kikwete, Kidongo Chekundu, Dar es Salaam na leo wanatarajiwa kuendelea na mazoezi Uwanja wa Taifa.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MECHI YA STARS NA WAHABESHI YAOTA MBAWA, VIJANA SASA KUPASHA TU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top