• HABARI MPYA

  Tuesday, October 04, 2016

  ISHA MASHAUZI NA LEYLA RASHID KUPAMBANA OKTOBA 22 DAR LIVE…Jahazi na Mashauzi Classic kusindikiza

  WAIMBAJI wawili wanaokimbiza kwenye soko la taarab kwa hivi sasa Isha Mashauzi na Leyla Rashid watapambana vikali Oktoba 22 ndani ya ukumbi Dar Live Mbagala.
  Unaambiwa ni malkia wawili ndani ya jukwaa moja, ambapo Isha Mashauzi atathibitsha kuwa nyeye ni malkia wa masauti matamu huku Leyla akitaka kudhihirisha kwamba yeye ndiye malkia wa taarab.
  Mratibu wa onyesho hilo Hajji Mabovu amesema bendi mbili kubwa za taarab Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic zitasindikiza mpambano huo wa Isha na Leyla.
  Waimbaji hao wawili kwa pamoja wameuthibitishia mtandao huu kuwa wamefikia makubaliano ya kuonyeshana ubabe Jumamosi ya tarehe 22 mwezi huu.
  Leyla Rashid amesema anamsikitikia sana Isha Mashauzi kwa kukubali kushiriki mpambano huo kwa vile kwasasa yeye (Leyla) ni maji marefu ambayo kamwe Isha hawezi kuyagoka.
  Naye Isha Mashauzi ametamba kuvuna ushindi mkubwa na kuongeza kuwa Leyla ameingia choo cha kiume kwa kukubali mtanange huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ISHA MASHAUZI NA LEYLA RASHID KUPAMBANA OKTOBA 22 DAR LIVE…Jahazi na Mashauzi Classic kusindikiza Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top