• HABARI MPYA

    Wednesday, June 01, 2016

    IHEANACHO APIGA BAO 'TAI KUBWA' LAUA 3-1 ULAYA, UGANDA WACHEZEA KICHAPO HARARE

    KINDA wa Manchester City, Kelechi Iheanacho amemalizia vizuri ziara ya timu yake ya taifa ya Nigeria barani Ulaya kwa kufunga bao katika ushindi wa 3-1 kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Luxembourg jana.
    Bao lake la kwanza akiichezea kwa mara ya kwanza timu ya wakubwa ya Nigeria, liliipa Super Eagles ushindi wa 1-0 dhidi ya Mali nchini Ufaransa Ijumaa iliyopita.
    Iheanacho, mfungaji wa mabao 14 kwenye mashindano yote ya msimu uliopita Man City, alifunga katika dakika ya 79 mjini Luxembourg City, hilo likiwa bao la pili kwa Nigeria katika mchezo huo, baada ya Brown Ideye wa Olympiakos ya Ugiriki kutangulia kufunga dakika tisa kabla ya mapumziko.

    Kelechi Iheanacho amemalizia vizuri ziara ya Super Eagles Ulaya kwa kufunga bao katika ushindi wa 3-1 jana

    Vincent Thill aliwashitua Wanigeria kwa kuwafungia bao la kwanza Luxembourg muda mfupi kabla ya mapumziko, lakini Odion Ighalo wa Watford akawafungia la tatu Super Eagles.
    Wakati timu kibao za Afrika zitakuwa na mechi za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika, wikiendi hii, Nigeria hawatakuwa mchezo baada ya Chad waliokuwa wacheze nao kujitoa katika Kundi G lenye timu za Misri na Tanzania pia, ambazo zitameyana Jumamosi Dar es Salaam.
    Mabao ya kipindi cha kwanza ya kinda Teenage Hadebe yameipa ushindi wa 2-0 Zimbabwe dhidi ya Uganda mjini Harare.
    Brian Mandela alifunga dakika ya nne kabla ya filimbi ya mwisho mjini Nairobi kuipa sare ya 1-1 Kenya dhidi ya Sudan, ambao walitangulia kwa bao Nizar Hamid.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: IHEANACHO APIGA BAO 'TAI KUBWA' LAUA 3-1 ULAYA, UGANDA WACHEZEA KICHAPO HARARE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top