• HABARI MPYA

  Wednesday, December 16, 2015

  YANGA SC KUREJEA KILELENI LIGI KUU LEO?

  RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
  Leo Desemba 16, 2015
  African Sports vs Yanga SC
  Desemba 19, 2015
  Yanga SC vs Stand United
  Mwadui FC vs Ndanda FC
  Kagera Sugar vs African Sports
  Prisons vs Mtibwa Sugar
  Toto Africans vs Simba SC
  Majimaji vs Azam FC
  Desemba 20, 2015
  JKT Ruvu vs Coastal Union
  Mbeya City vs Mgambo JKT
  Desemba 23, 2015
  Azam FC vs Mtibwa Sugar
  Desemba 26, 2015
  Ndanda FC vs JKT Ruvu
  Yanga SC vs Mbeya City
  Majimaji vs Prisons
  Mwadui FC vs Simba SC
  Mtibwa Sugar vs Mgambo JKT
  Coastal Union vs Stand United
  Desemba 27, 2015
  Azam FC vs Kagera Sugar
  Toto Africans vs African Sports

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kwa mchezo mmoja tu, mabingwa watetezi, Yanga SC wakimenyana na wenyeji African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
  Yanga SC inahitaji ushindi katika mchezo wa leo, ili kurejea kuleleni mwa ligi hiyo baada ya kuenguliwa na Azam FC mwezi uliopita.
  Na kocha Mkuu wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm amesema kurejea kwa kinara wake wa mabao, Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma kunamjaza matumaini ya ushindi leo.
  “Kama unavyojua, Ngoma ndiye mfungaji bora wa timu, kumkosa katika mchezo wetu uliopita lilikuwa pigo kubwa, tunashukuru sasa tutakuwa naye tena,”amesema Pluijm.
  Ngoma alikosekana Jumamosi Yanga SC ikilazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji, Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani.
  Kwa sasa, Ngoma ana mabao nane katika Ligi Kuu sawa na mshambuliaji wa Simba SC, Mganda Hamisi Kizza ‘Diego’, wote wakizidiwa bao moja na mshambuliaji wa Stand United, Elias Maguri – wakati Muivory Coast, Kipre Herman Tchetche wa Azam FC anawafuatia akiwa na mabao saba na Mrundi Amissi Tambwe wa Yanga ana mabao matano sawa na John Raphael Bocco wa Azam FC na Ibrahim Hajib wa Simba SC.
  Yanga SC kwa sasa inashika nafasi ya pili katika Ligi Kuu kwa pointi zake 24, baada ya kucheza mechi 10, nyuma ya Azam FC yenye pointi 26 za mechi 10 pia, wakati Mtibwa Sugar yenye pointi 23 ni ya tatu na Simba ni ya nne kwa pointi zake 22 baada ya timu zote kucheza mechi 10 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC KUREJEA KILELENI LIGI KUU LEO? Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top