• HABARI MPYA

    Saturday, December 26, 2015

    YANGA SC RAHA HADI MWAKA MPYA, MBEYA CITY AFA 3-0 TAIFA, SIMBA SARE 1-1 NA JULIO

    Wachezaji wa Yanga SC wakifurahia bao lao la tatu leo dhidi ya Mbeya City
    YANGA SC imetanua mbawa kileleni mwa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Ushindi huo unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 33, baada ya kucheza mechi 13, wakati Azam FC iliyocheza mechi 12, ina pointi 29.
    Mrundi Amissi Tambwe aliifungia Yanga SC mabao mawili mfululizo, la kwanza dakika la 37 akimalizia pasi ya winga Simon Msuva na la pili dakika ya 65 akimalizia krosi ya Mwinyi Hajji Mngwali, kabla ya kumpasia kwa kichwa Mzimbabwe Thabani Kamusoko kufunga la tatu dakika ya 
    66.
    katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, Simba SC imelazimishwa sare ya 1-1 na Mwadui FC ya kocha Jamhuri KIhwelo ‘Julio ’Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
    Mwadui walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Nizar Khalfan dakika ya 77, kabla ya Brian Majwega kuisawazishia Simba SC dakika ya 86.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC RAHA HADI MWAKA MPYA, MBEYA CITY AFA 3-0 TAIFA, SIMBA SARE 1-1 NA JULIO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top