• HABARI MPYA

  Tuesday, December 15, 2015

  NONGA ASAINI MIAKA MIWILI YANGA SC, GARBA ASAINI MWAKA MMOJA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  RASMI. Paul Nonga (pichani kushoto) na Issoufou Boubacar Garba ni wachezaji wa Yanga SC, baada ya wawili hao wote kusaini mikataba makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam.
  Nonga amesaini Mkataba wa miaka miwili akitokea Mwadui FC, ambayo ameichezea kwa miezi mitano tu tangu ajiunge nayo kutoka Mbeya City.
  Na mchezaji huru kutoka Niger, Garba amesaini Mkataba wa mwaka mmoja, wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja, iwapo atafanya vizuri.
  Winga wa zamani wa Club Africain na ES Hammam-Sousse za Tunisia, Garba aliyezaliwa mji wa Niamey, mwenye urefu wa futi 5 na inchi 6, kisoka alianzia klabu ya AS FAN ya kwao mwaka 2010, kabla ya kuhamia Thailand ambako alichezea klabu za Muangthong United mwaka 2011 na Phuket.
  Paul Nonga akiwa ofisi ya Katibu Mkuu wa Yanga SC, baada ya kusaini Mkataba jioni ya leo
  Mwaka 2012 alitua Club Africain ya Tunisia ambako hakucheza mechi hadi anahamishiwa 
  ES Hammam-Sousse ambako pia hakucheza.
  Wasifu wake unaonyesha tangu ameondoka ES Hammam-Sousse hajapata timu nyingine, lakini uongozi wa Yanga SC umejiridhisha alikuwa anachezea klabu bingwa ya kwao, AS Douanes.

  Garba amesaini Mkataba wa mwaka mmoja, wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja, iwapo atafanya vizuri
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NONGA ASAINI MIAKA MIWILI YANGA SC, GARBA ASAINI MWAKA MMOJA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top