• HABARI MPYA

  Tuesday, December 15, 2015

  HABARI NJEMA AZAM FC, AGGREY, MWANTIKA NA DIOUF WAANZA MAZOEZI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MABEKI watatu wa kati wa Azam FC waliokuwa majeruhi, Aggrey Morris, David Mwantika na Msenegali Racine Diouf wameanza mazoezi leo baada ya kupata ahueni.
  Watatu hao walikosekana wakati Azam FC ikilazimishwa sare ya 2-2 na Simba SC Jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na ikaonekana kabisa makosa ya safu ya ulinzi yaliwapa mabao wapinzani kiulaini. 
  Mabeki hao jana walipewa programu maalumu ya kufanya mazoezi ya viungo gym, ambapo walikuwa wakisimamiwa kwa ukaribu na Kocha wa Viungo, Adrian Dobre.
  Na vinara hao wa Ligi Kuu wanatarajia kuingia kambini kesho mchana katika hosteli za Azam Complex kujiandaa na mchezo wao ujao dhidi Majimaji Jumapili wiki hii mjini Songea.
  Aggrey Morris amerejeaa mazoezini Azam FC baada ya kukosa mechi dhidi ya Simba SC

  Kocha Mkuu wa Azam FC, Muingereza Stewart John Hall amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba, programu ya mazoezi ya kesho itakuwa ni jioni na watafanyia kwenye Uwanja wa Chuo cha Ualimu Dar es Salaam (DUCE).
  “Tumepata Uwanja unaoendana na ule wa Majimaji, tunaoenda kuchezea mechi, programu itakuwa tutafanyia Jumatano (kesho) na Alhamisi (keshokutwa),” alisema.
  Amesema timu itaondoka Ijumaa asubuhi kwa ndege kwenda Mbeya ambako watakutana na basi lao, wakalolitumia kuingia Songea.
  Azam FC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 26, baada ya kushinda mechi nane na sare mbili, imefungwa jumla ya mabao saba na kufunga 22, ikifuatiwa na Yanga pointi 24, Mtibwa Sugar 23 na Simba 21.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HABARI NJEMA AZAM FC, AGGREY, MWANTIKA NA DIOUF WAANZA MAZOEZI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top