• HABARI MPYA

    Thursday, December 19, 2019

    YANGA YAPANGWA KUNDI MOJA NA AZAM FC, SIMBA NA MTIBWA SUGAR KOMBE LA MAPINDUZI 2020

    Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
    YANGA SC imepangwa Kundi A pamoja na mabingwa watetezi, Azam FC, zote za Dar es Salaam, Jamhuri ya Pemba na Mlandege ya Unguja kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza Januari 5 hadi 13 mwakani, ikishirikisha timu za Bara na Visiwani.
    Washindi wa pili msimu uliopita, Simba SC wapo Kundi B pamoja na Mtibwa Sugar zote za Bara, Zimamoto na Chipukizi za Zanzibar. 
    Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Zanzibar imeitangaza Kamati ya kusimamia Mashindano ya Kombe la Mapinduzi na tarehe ya kuanza Mashindano hayo ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
    Katika taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara hiyo Omar Hassan Omar ‘King’ mashindano hayo yanatarajiwa kuanza January 5, 2020 na kumalizika January 13, 2020 ambapo jumla ya timu 8 zinatarajiwa kushiriki Mashindano hayo ambayo yatachezwa kwenye viwanja vya Gombani Kisiwani Pemba na Uwanja wa Amaan Kisiwani Unguja.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi ni Sharifa Khamis Salim na Katibu wa Kamati hiyo ni Khamis Abdulla Said.
    Wajumbe wa Kamati ni Khamis Mussa Omar, Issa Mlingoti, Seif Kombo Pandu, Mohamed Ali Hilali (Tedy), Aiman Othman Duwe, Fatma Hamad Rajab, Salum Ubwa Ali Khalil, Juma Mmanga na Suleiman Pandu Kweleza.
    Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza January 5, 2020 na kumalizika January 13, 2020 mashindano hayo yatachezwa kwenye viwanja vya Gombani Kisiwani Pemba na Uwanja wa Amaan Kisiwani Unguja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA YAPANGWA KUNDI MOJA NA AZAM FC, SIMBA NA MTIBWA SUGAR KOMBE LA MAPINDUZI 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top