• HABARI MPYA

    Monday, December 23, 2019

    DIRISHA DOGO ANASAJILIWA NDAMA BADALA YA NG'OMBE WA MAZIWA!

    Na Mustafa Mtupa, DAR ES SALAAM
    WAKATI nikiwa nipo likizo baada ya mihangaiko ya takribani miezi kadhaa kazini nikiwa nimeenda kijijini kidogo kumsalimu Babu na Bibi.
    Moja ya masiku nikiwa nimeketi na babu kwenye jamvi kukuu kuu lililo pambwa na matobo matobo ya kuashiria uchovu wake kwa kukaliwa mda mrefu. Nikiwa natazama juu namna ambavyo nyota zimeganda angani na kimoyo moyo nikajiemea kwamba  hakika mungu ni fundi.
    Wakati nikiwa hapo nilijikuta napata shauku ya kudadisi jambo kuhusiana na mnyama aina ya Ng'ombe kutoka kwa Babu kwakuwa alikuwa akiwafuga.
    Nilimuuliza Babu kwamba Ndama ndo ng'ombe wa aina gani?Akanijibu kwa kusema kuwa Ndama ni Ng'ombe mdogo ambaye akikua ndo tunamwita Ng'ombe kwaiyo Ndama ni mtoto wa Ng'ombe.

    Baada kupewa kauli ileee nikajikuta nakumbuka kinacho endelea kwenye Dirisha dogo la usajili kunako Ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara.
    Picha iliyo nijia kichwani ni aina ya ndama ambao mpaka sasa wamezaliwa kwenye dirisha hilo, huku wenye hao ndama wakiamini kuwa hawajasajili ndama bali ni Ng'ombe aliyekamilika.
    Kwa kawaida Ndama huwa anahitaji kukua na kuzoea Mazingira ili aje kuwa Ng'ombe kamili.
    Kwa kawaida kuna utofauti kati ya Ndama mmoja na mwengine kwenye kuyazoea mazingira na hata ukuaji. sawa tu na ulivyo utofauti kati ya mchezaji mmoja na mwengine kuna baadhi ya wachezaji huwa wana ingia haraka  kwenye mfumo na kuonyesha kiwango bora, lakini pia kuna wachezaji ambao huchelewa kuendana na mazingira na kuingia kwenye mfumo wa timu kwa haraka na hivyo huitaji mda ili kutoa walicho nacho.
    Ndama hawa wanaohitaji mda ndio huchinjwa kwakuwa watu walio wanunua waliowengi hawaitaji kusubiri kwani vichwani mwao walishaweka matumaini ya kuwa hawa ni Ndama watakaokuwa Ng'ombe baada ya siku mbili tu, wakati ndama hawa walihitaji miezi na miezi ili kuwa Ng'ombe kamili.
    Wamiliki hawa wamesahau kwamba kwa kipindi hiki ule misimu wa majani mengi ama Pre season haupo hivyo kuna baadhi ya hawa wachezaji walio wasajili  hawatakula lishe ya kutosha ya kuwafanya watoe asilimia zoote uwanjani.
    Dirisha hili ni dirisha ambalo limekuwa na matokeo mengi mabovu katika sajili zinazo fanywa,kwa sababu wachezaji wengi huwa wanashindwa kuingia kwenye timu kwa haraka na wakati huo wenye timu zao waliwasajili kama suluhisho la tatizo na badala yake inakuwa kinyume chake kwamba suluhisho la tatizo ndo huleta Tatizo.
    Moyo huniingia ganzi ninapoona baadhi ya wachezaji wanashindwa kucheza vizuri baada ya kusajiliwa katika dirisha hili na kuonekana kama ni watu waliofeli kabisa baada ya mechi kadhaa tu.
    Rai yangu kwa watu wenye mamlaka ni kuwa wachezaji wanaosajiliwa katika kipindi hiki huwa wanakumbwa na kadhia kubwa ya mashabiki kuwahitaji waoneshe walichonacho kwa mda mfupi saana hali inayo wapelekea wao kuingiwa na shinikizo na hata wakapotea kabisa kwani saikolojia yao nayo huwa imeharibika.
    Muda na umakini ndio mambo peke yatakayo wafanya ndama munao wasajili leo kuwa Ng'ombe kesho.lakini kama mutashindwa kuvifata vitu hivi nawaona Ndama hawa wakichinjwa kabla hata ya kunywa hata maji.
    Kiza nacho kilianza kutanda ikabidi ninyooshe mgongo na niachane na haya maswali ya Ndama na Ng'ombe kwani babu alishachoka naye.
    (Mwandshi wa makala haya ni Kalamu nyeusi na unaweza kumpata  @insta,MtotoWamkulima99. @facebook:Mustafa Abainder au nambari ya simu + 255 687 058 966)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DIRISHA DOGO ANASAJILIWA NDAMA BADALA YA NG'OMBE WA MAZIWA! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top