• HABARI MPYA

    Friday, December 20, 2019

    BEN POL ATOA ZAWADI YA KRISMASI KWA MASHABIKI WAKE, NI WIMBO MPYA UITWAO SIKUKUU.

    Na Asha Said, DAR ES SALAAM
    MKALI wa R&B nchini Benard Paul 'Ben Pol' ametoa zawadi ya Krismasi kwa mashabiki wake baada ya kuachia kibao kipya kinachoitwa Sikukuu.
    Ben Pol ameachia nyimbi hiyo mapema wiki hii ikiwa ni maalumu kwa mashabiki wake na ukiwa ni wimbo maalumu wa sikukuu.
    Kwa upande Ben Pol amesema, ameamua kuutoa wimbo huu ukiwa ni kama zawadi ya sikukuu kwa mashabiki zake ili uweze kuwaburudisha katika kipindi chote cha Sikukuu za Krismasi na mwaka mpya.
    Amesema, wimbo huo ameutengeneza kwa Producer Tiddy Hotter Kwenye studio za  One Love Records huku upande wa Video akisimama mkongwe Adam Juma.
    "Wimbo huu ww nimeupa jina jina la sikukuu kwa kuwa ni zawadi kwa mashabiki zangu, na jana rasmi niliweza kuuachia Audio na Video, zote kwa pamoja,"amesema
    Aidha, Ben Pol amesema anaamini mashabiki wake wataupokea vyema wimbo wake huu mpya alioutoa mahususi kwa ajili yao.
    Msanii huyo, anayeimba miondoko ya R n B amekuwa katika muendelezo mzuri wa Kisanii baada ya hivi karibuni aliweza kushirikishwa wimbo wa Nipokeeni ulioimbwa ba Chid Benz, huku kwa upande wake nyimbo zake za Wapo na Sana bado zikiendelea kufanya vizuri.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BEN POL ATOA ZAWADI YA KRISMASI KWA MASHABIKI WAKE, NI WIMBO MPYA UITWAO SIKUKUU. Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top