• HABARI MPYA

    Thursday, December 19, 2019

    UGANDA WAIPIGA ERITREA 3-0 NA KUTWAA KOMBE LA CHALLENGE

    Na Mwandishi Wetu, KAMPALA
    UGANDA wamefanikiwa kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Eritrea jioni ya leo Uwanja wa Lugogo mjini Kampala.
    Ushindi huo wa taji la 15 na mara 40 jumla tangu enzi za Gossage kwa Uganda umetokana na mabao ya Bright Anukani wa Proline FC dakika ya 31, Mustafa Kizza wa KCCA FC dakika ya 68 na Joel Madondo wa Busoga United dakika ya 88.
    Na baada ya mechi, Charles Lukwago wa The Cranes akapewa tuzo ya Kipa Bora wa Mashindano, Robel Tekle Michael wa Eritrea Mchezaji Bora na Mfungaji Bora ni Oscar Wamalwa wa Kenya.

    Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Kenya iliichapa Tanzana Bara 2-1 na mchana wa leo Uwanja wa Lugogo mjini Kampala.
    Kenya iliyo chini ya kocha Francis Kimanzi, iliuachia ubingwa wa Challenge baada ya kuchapwa 4-1 na Eritrea juzi ambao leo wanateremka uwanjani kumenyana na wenyeji, Uganda katika fainali.
    Na leo Harambee Stars ikafanikiwa kumalizia hasira zake kwa Kilimanjaro Stars kwa kuwachapa 2-1, mabao ya Kenya yakifungwa na Kenneth Muguna dakika ya 16 akimalizia pasi ya Oscar Wamalwa na Hassan Abdallah dakika ya 36 akimalizia pasi ya Lawrence Juma.
    Na Tanzania Bara chini ya kocha wake, Juma Mgunda ikafanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika ya 82 kupitia kwa beki wake wa kushoto, Gardiel Michael aliyefungwa kwa penalti dakika ya 82 baada ya kiungo Hassan Dilunga kuangushwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UGANDA WAIPIGA ERITREA 3-0 NA KUTWAA KOMBE LA CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top