• HABARI MPYA

  Wednesday, December 12, 2018

  YANGA KUANZA NA IHEFU AU TUKUYU STARS, AZAM NA MADINI AU STAND BABATI, SIMBA SC NA MASHUJAA KOMBE LA TFF

  RATIBA KAMILI AZAM SPORTS FEDERATION CUP 
  Namungo FC v Sahare All Stars/Deportivo
  Geita Electrict/Kamuyange v Kagera Sugar
  Mtibwa Sugar v Kiluvya United
  Lipuli FC v Laela FC/Mitumba FC  
  Stand United v Ashanti United
  Changanyikeni/Barger FC v Coastal Union
  Reha FC v Zakhem/Mkamba Rangers
  Maji Maji FC v Toto Africans/Gipco
  Boma FC v Njombe Mji FC
  Pan African /Villa Squad v Mwadui FC
  Cosmopolitan v Green Warriors 
  Rhino Rangers v Nyamongo FC/Bulyanhulu FC
  Azam FC v Madini FC/Stand Babati
  KMC v Tanzania Prisons
  Kilimanjaro Forest /Kilimanjaro Heroes v Polisi Tanzania
  Moro Kids/Maji Maji Rangers v Mbeya Kwanza 
  Geita Gold FC v Biashara United 
  Ruvu Shooting v Mucoba FC/Might Elephant 
  Yanga SC v Ihefu FC/Tukuyu Stars
  Singida United v Arusha FC 
  Sharp Striker/Usalama v Friends Rangers 
  Dodoma FC v Kasulu Stars/Home Boys
  Mufindi United v Alliance FC
  Mbeya City v Mgambo Shooting 
  African Lyon v Arusha United 
  Simba SC v Mashujaa FC (Kigoma) 
  La Familia/Area C v Mawenzi Market 
  Mbao FC v Dar City 
  Stand Dortmund/Milambo FC v JKT Tanzania  
  Mtwivila/Livingston v Pamba FC 
  Ndanda FC v Trans Camp
  Mnale FC v Kitayose/African Sports
  (Mechi zitachezwa kuanzia Desemba 21 hadi 24, 2018)
  Mtibwa Sugar iliifunga Singida United 3-2 na kutwaa taji la Azam Sports Federation Cup Juni 2, mwaka huu Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha  

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  VIGOGO, Azam, Simba na Yanga wote wataanzia nyumbani hatua ya 64 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ijulikanayo kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
  Hiyo ni baada ya droo ya raundi ya tatu ya michuano hiyo, iliyofanyika leo makao makuu ya Azam TV, hapa Tabata, Dar es Salaam ikishuhudiwa KMC NA Tanzania Prisons kuibuka mchezo pekee utakaokutanisha wapinzani wa Ligi Kuu watupu.
  Azam FC watakuwa wenyeji wa ama Madini FC ya Arusha, au Stand ya Babati, Yanga SC wataikaribisha amaIhefu FC au Tukuyu Stars, zote za Mbeya na Simba SC watawaalika Mashujaa FC kutoka mkoani Kigoma.
  Mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar wao wataanza na Mtibwa Sugar na Kiluvya United ya Pwani Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro, wakati washindi wa pili Singida United wataanzia nyumbani pia Uwanja wa Namfua mkoani Singida dhidi ya Arusha FC. 
  Mechi zitachezwa wikiendi ijayo kuanzia Desemba 21 hadi 24 na hii moja kwa moja inamaanisha mechi itachezwa kabla au baada ya mchezo wa marudiano wa Simba na Nkana Desemba 23 Dar es Salaam, lakini mabingwa wa Tanzania Bara wanajivunia kikosi kipana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA KUANZA NA IHEFU AU TUKUYU STARS, AZAM NA MADINI AU STAND BABATI, SIMBA SC NA MASHUJAA KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top