TIMU ya Simba SC imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji FC jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arisha.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji Suleiman Abdallah Mwalimu mawili dakika ya 54 na 67 na winga wa kushoto Muivory Coast, Alain Anicet Oura dakika ya 60 baada ya kiungo Khleffin Salum Hamdoun kuanza kuifungia Dodoma Jiji FC dakika ya tisa.



.png)
0 comments:
Post a Comment